Ushuda wa kweli

Dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahida,
alikuwa anafanya biashara ya kujiuza ili aweze
kuweka kitu umboni mwake. dada huyo alikuwa
na wateja wamaana na mapedeshee wengi sana
kwa hiyo kwa siku yeye kuondoka na laki 4 au 5
kwa siku ilikuwa ni kawaida sana. siku moja dada
Mahida aliamua aende hospitali ili akatoe miamba
aliyokuwa nayo tumboni mwake, alifanikiwa na
kutoa mimba ile lakini baada ya kumaliza utoaji
wa miamba alimuomba daktari atoe kizazi kabisa
ili asipata tabu ya kuja kutoa mimba kila mara,
daktari alifanya kama alivyoambiwa.
Dada Mahida alirudi mtaani na kuendelea na
biashara ya kujiuza.
Siku moja ilikuwa jumapili Mahida alikutana na
rafiki yake wa muda mrefu waliyekuwa wanaishi
wote enzi za utoto wao, rafiki yake huyo
alimwambia Mahida waende kanisani, ili kuficha
aibu ya biashara aliyokuwa anafanya dada
Mahida alikubari na wakaamua kwenda wote
kanisani. Siku hiyo Mahida alielewa sana neno na
akaahidi kuwa jumapili ijayo ataenda, basi ikawa
tabia mpya ya dada Mahida akawa kila siku
anafanya biashara zake za kujiuza na jumapili
anaenda kanisani, kadri siku zinavyozidi kwenda
dada Mahida akaanza kupunguza biashara ya
kujiuza na kumgeukia Muumba mpaka akaacha
kabisa tabia ya kujiuza na kuanza kufanya
shughuli nyingine zilizokuwa zinamuingizia kipato.
Siku moja Mahida alienda kanisani na alipokuwa
ameketi mchungaji alimfuata na kumwambia
“nimeoteshwa kuwa ww ndiyo utakuwa mke
wangu wa kufa na kuzikana” dada Mahida
alishtuka na alimtazama mchungaji na
kumwambia “mchungaji umekurupuka mimi
kamwe siwezi kuwa mke wa mtu na kamwe siwezi
kuzaa” alimaliza Mahida na kuondoka kanisani,
kila wiki aliyokuwa anaenda kanisani dada Mahida
alikutana na maneno yale yale kwa mchungaji na
mchungaji alimwambia “nimeota umepata ujauzito
na umenizalia watoto wanne” Mahida
alimuangalia mchungaji na kusimama na
msimamo wake ulele ule.
Siku zilizidi kuyoyoma lakini kutokana na
mchungaji kuendelea kusema maneno yale yale
basi ilibidi dada Mahida akubali na akakubali
kuolewa na mchungaji na wakafunga ndoa na
ndoa yao ilikuwa ya furaha sana. kadri siku
zilivyozidi kwenda dada mahida alianza kuona
mabadiliko mwilini mwaka na kuamua kwenda
katika ile hospitali aliyowahi kwenda mwanzo
kutoa mimba na kumkuta daktari aliyemfanyanyia
utoaji wa mimba siku za nyuma, baada ya daktari
kumona Mahida akajua amkekuja kwa shida
nyingine ikabidi amuulize “Dada Mahida
nikusaidie nini tena dada yangu” mahida alijibu
kuwa anahisi anadalili za ujauzito, Daktari alicheka
sana baada ya kuambiwa hayo majibu kutoka kwa
mahida na daktari alimwambia “Dada mahida
nona umechanganyikiwa enh dada yangu?? mimi
ndiye nilitoa kizazi chako leo iweje uwe na mimba
acha kuchekesha walionuna”
Mahida alimwambia daktari chukua vipimo
kapime, kweli daktari alifanya hivyo na baadae
akarudi mikono inamtetemeka na kumwambia
mahida “Dada Mahida nipeleke na mimi kwa
huyo uneyebuabudu nami niweze kumuabudu
maana ni mkweli na anasaidia wanyonge, Dada
Mahida ww ni mjamzito wa miezi miwili”. Mahida
alilia huku akiamini kuwa Mungu ashindwi na kitu
chochote Duniani.
Daktari wiki ilifata naye alienda kanisani na
kuanza kumtukuza muumba.
Ndugu yangu hata kama upo katika wakati
mgumu kiasi gani lakini kumbuka yupo anaweza
kufanya ugumu wa mambo yako kuwa mepesi
kama unatafuna karanga.
hakunna kinachoshindikana kwa Mungu,
comment AMINA kama unaamini hakuna
kinachoshindikana kwa jina lake yeye muumba na
kama unaamini magumu yako yote yenaweza
kuwa mepesi kupindukia.
Share na mwenzako kufikisha ujumbe.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to Ushuda wa kweli

 1. Sophia Dickson Mhando says:

  Amen

  Like

 2. What’s up, I log on to your blog regularly. Your story-telling style is awesome,
  keep doing what you’re doing!

  Like

 3. kutokana na haya,je pastor aliingia kwe nye huduma bila mke? mmh ina wezekanaje?

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s