Mtume baraza ampinga Gwajima kuhusu misukule

® Adai kurudisha misukule kila crusade ni mchezo wa kichawi

@ Amtaka ampeleke nchini Haiti akashindane na wachawi wa huko

Misukule ni nini? Ni watu ambao hufa wakazikwa lakini sio kifo cha ukweli ni kifo cha kichawi ambapo wachawi wanafumba watu macho. Na mtu aliekufa huwa anapelekwa kulima mashamba. Wachawi wana uwezo wakuwateka watu kuwapeleka musukule ama kuwarudisha kwa nguvu za giza.

Mimi sipingi kwamba watu wa Mungu hawawezi kurudisha mtu toka msukule.Lakini ninachopinga ni kwamba haiwezi kuwa ni kila siku nenda rudi ni kurudisha misukule

Misukule ni disco na dansi ya wachwi. Na Mungu hawezi cheza mchezo huu na shetani kila siku kwani Yesu alishinda kifo mara moja wala haitaji kushindana na wachawi wa Misukule kila siku ili kuonyesha ana nguvu juu ya mauti.

Alishinda mauti mara moja aliposema imekwisha UFUNUO 1-18 Mimi ni Alfa na Omega Mwanzo na Mwisho, nilikuwa nimekufa na sasa Tazama niko mzima hata milele ninazo funguo za Uzima na mauti

Kumbuka Mungu hafanyi kazi kwa mwelekeo moja. Inapofika mhubiri kubuni Injili ya misukule inageuka na kuwa dini maana Roho wa Mungu ni kama upepo anafanya kazi kwa njia mbalimbali.

Mtu wa Mungu anaweza kutumiwa kurudisha msukule mara kadhaa lakini hawezi kudai kwamba YEYE NISPECIALIST WAKURUDISHA WAFU WA MISUKULE EVERY DAY, EVERY CRUSADE HIYO NI MCHEZO WA KICHAWI mchezo huu unafanywa kwa wingi nchi ya HAITI ambapo wachawi huwapiga watu kufa kifo cha kimapepo hata siku 20 ambapo mtu anaonekana amekufa anazikwa halafu baada ya siku 10, 20,30,40 wachawi wanakuja kaburini mchana peupe na wanamfufua mfu.

NAWABIENI KAMA MTUME WA YESU KRISTO.

MUNGU HAYUMO KWENYE MCHEZO WA MISUKULE KILA SIKU NENDA RUDI HIYO NI DISCO NA NI NGOMA YA SHETANI. NI MCHEZO AMBAPO WACHAWI WANAJARIBU KUONYESHA WANA NGUVU JUU YA KIFO. SISI WAKRISTO TUNAJUA YESU AMESHINDA KIFO MARA MOJA NA WALA HATARUDIA KAMWE.

Ishara nyingine za manabii wa Uongo hizi hapa:

Wanauza mafuta, Vitambaa, Funguo, picha, udongo, kofuli, mishumaa, wanapenda pesa, wanaishi maisha a kifahari, wana kiburi tena wanadai wao ndio besy of the best

Akijibu swali la ndugu Frank Daniel aliloandika kutoka Isaya 42:22 “lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye, RUDISHA. kumbe kuna watu walioibiwa na kutekwa na hakuna awaokoae wala arudishaye”

Mtume Baraza akajibu “Mashimo na magereza ni mengi ndugu Frank andiko hili liko applicable kwa sehemu nyingi kama kwa mfano kuna gereza na mashimo mbalimbali kama ukahaba, ulevi, uchawi, wizi nakadhalika wala huwezi kulifanya misukule pekee.

Zaburi 40 Daudi anasema Nalimgoja Bwana kwa subira akanitoa toka shimo la uharibifu. Daudi alikuwa shimoni wa msukule

Isaya 58 Ukisoma inataja vifungu vya nira na kongwa mbali mbali kwahiyo andiko ulilotoa linazungumza juu ya nira aina nying halizungumzii msukule pekee.

Amini usiamini nakwambia kama mtume wa Kristo ni makosa kwa mhubiri yeyote kuhubiri misukule mkoa kwa mkoa mkutano kwa mkutano. Hiyo ni confusion na ni upotovu na nimafundisho yasiyo ambatana na Kristo.

Ikiwa Gwajima anahuduma ya Misukule mbona asiende nchi ya Haiti huko kuna wachawi wanachukua watu misukule mchana sokoni hawajifichi. Huduma yake itapamba moto huko

Mbona asiende huko kuna watu maelfu misukule hadharani mchana.

Ikiwa yuko tayari nitamnunulia ticketi ya ndege nimlipie hoteli miezi sita twende naye huko nchini Haiti arudishe misukule, yaani watu wasiokoke lakini kila siku akiamka tunaenda naye sokoni Haiti kupambana na wachawi wanaoteka misukule na Gwajima anarudisha, ikifika jioni tunaenda kulala asubuhi ikifika tunakunywa chai tunaenda sokoni.

Sijui kama mnaipata point yangu? Je hii ndio Injili Yesu ametutuma tuhubiri kila siku? Kuchalenge wachawi ama tuhubiri watu waokolewe?

Naomba majibu labda nimechanganyikiwa!!

–Mtume Augustus Baraza Matibila

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

5 Responses to Mtume baraza ampinga Gwajima kuhusu misukule

 1. Filbert Mmari says:

  Yesu mwenyew alitahadharisha juu ya ujio wa manabii na makuhani wa uongo..akaagiza kwamba,tusiwasikilize hao bali tuifuate kweli yake nayo itatuweka huru kweli kweli..injili ya kweli is ya mazoea bali ni yakuleta uponyaji wa kweli,ili watu wamwogope Mungu na kumpenda siku zote za maisha yetu.. Tujihadhari sana na matukio kama hayo siku hizi za mwisho.

  Like

 2. ukweli utajurikana tu yesu si anarudi.

  Like

 3. SEM DEDE. says:

  kaaaa. mtume hilo ni jiwe la shingo. hv mnayajuaje mambo haya ?

  Like

 4. Mtumishi says:

  Unashangaza sana,yeremia 1:10 unaielewaje ? Je yohana 14:12-14’unaielewa vilivyo ? Ya nini kupingana na watumishi wa Mungu ? Wewe eti mtume ajabu…ajidhaniaye amesimama aangalie asije akaanguka.kila mmoja ameitwa kwa kazi yake.Biblia ni pana sana ila mfumo wa kuielewa kwa mapokeo ya madhehebu mlikotokea ni vigumu.kila mmoja kapokea sehemu ya mwili wa Kristo maana tu viungo ktk mwili wa Kristo.Kwa taharifa yako sio misikule tu,na magonjwa mengi wameponywa. Ha ha ha kama unaye Mungu wako mtambulishe uwezavyo
  ‘Hata mimi naombea watu.soma uelewe ufunuo 5:1-10.Ndug tunayaweza haya yote ktk yeye .lakini sishangai sana maana siku hizi shetani anafanya kazi na wanadamu,kweli shambani mwa Bw watendakazi ni wachache.shughulika nakazi ulio Iitiwa.niko Bukoba

  Like

 5. Mtumishi Fredy says:

  Unashangaza sana,yeremia 1:10 unaielewaje ? Je yohana 14:12-14’unaielewa vilivyo ? Ya nini kupingana na watumishi wa Mungu ? Wewe eti mtume ajabu…ajidhaniaye amesimama aangalie asije akaanguka.kila mmoja ameitwa kwa kazi yake.Biblia ni pana sana ila mfumo wa kuielewa kwa mapokeo ya madhehebu mlikotokea ni vigumu.kila mmoja kapokea sehemu ya mwili wa Kristo maana tu viungo ktk mwili wa Kristo.Kwa taharifa yako sio misikule tu,na magonjwa mengi wameponywa. Ha ha ha kama unaye Mungu wako mtambulishe uwezavyo
  ‘Hata mimi naombea watu.soma uelewe ufunuo 5:1-10.Ndug tunayaweza haya yote ktk yeye .lakini sishangai sana maana siku hizi shetani anafanya kazi na wanadamu,kweli shambani mwa Bw watendakazi ni wachache.shughulika nakazi ulio Iitiwa.niko Bukoba

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s