Baadhi ya wanasiasa wanajihusisha na mauaji ya albino!!

Zeru 1Shalom, ikiwa watu wengi sana wametia mikono yao kuandika na kupaza sauti zao kuhusu haya mauaji ya walemavu wa ngozi yaani zeruzeru.

Nami leo baada ya kuwa kimya sana nimeamua kusema.

kwa ujumla lawama zinawaendea sana wafanyabiashara na waganga wa kienyeji. lakini ukweli bila kupinda ni kwamba waganga wa kienyeji na wachawi ndiwo chanzo kizima cha mauji haya. lakini swali la kujiuliza hawa waganga na wachawi wanavifanyia kazi gani hivi viungo vya albino! inasemakana kwamba huwatengenezea dawa wateja wao ili wafanikiwe katika mambo mbali mbali ya kijamii, kiutawala na kisiasa yakiwemo kupata utajiri na madaraka.

waziri mkuu mstaafu fredrick sumaye tulimkaribisha kanisani kwetu juzi, aliikemea hii tabia akisema “unawakata albino mikono ili upate utajiri na madara” kauli hii ya waziri ilinifumbua macho, mimi nilidhani zeruzeru wanauwa na wafanya biashara ili kwamba biashara zao ziende mbele. lakini kumbe wanauawa pia na wanasiasa ili wapate madaraka.

katika hilo la madaraka mimi naona ni chanzo kikubwa cha vifo vya watu hawa, na serikali haitaweza kulidhibiti maana kama hiyo ndiyo dhana basi viongozi wa juu wa serikali wanahusika!

kwa kweli nafikiri sumaye alikuwa sahihi kabisa kwamba wanauawa ili watu wapaate madaraka, na ndio maana nashangaa kwamba haya mauaji huwa yanapamba moto wakati na kipindi cha uchaaguzi unapokaribia tu, baada ya uchaguzi utaona mambo shwari, albino watatembea hata saa nane usiku. lakini uchaguzi ukikaribia albino wanaishi kama swala wa serengeti, muda wote wanawindwa, hata kulala kwao hulala kwa kujihami na maombi mengi ili Mungu awatetee.

jamani hii nchi ni yetu sote, bila kujali albino au character ya mtu. kama wewe unataka kuwa kiongozi wakati huo huo unawaangamiza watu ambao ungekuwa kiongozi wao, sasa utamwongoza nani? mimi nafikiri serikali kupitia idara ya usalama wa taifa ingeunda tume rasmi ya kuwachunguza viongozi wote na wagombea wote kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa. hii itatusaidia kubaini ni nani anayehusika na haya mambo, si ajabu ukakuta kwamba anayeagiza waganga wa kienyeji wakamatwe ndiye anayehusika na haya mambo.

Kiongozi yeyote anayehusika na mauji haya. mimi natamka hivi sio kama moses tena, bali kama mtumishi wa Mungu niliyepewa mamlaka kutoka juu. nasema kwamba Mungu akutane na huyo kiongozi au mwanasiasa yeyote anayetenda au kujihusisha kwa namna moja ama ningine na matendo ya kikatili kama haya, na Mungu akikutana naye asikutane naye kama rafiki bali ambane kiasi kwamba ajute kutenda hayo, ila namwomba Mungu akukumbuke kwenye ufalme wake. akuadhibu ila asikutupe jehanam.

“MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU ITETEE TANZANIA”

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s