YEZEBELI HAUAWI KWA UPAKO

Yezebeli hatafutwi kwa kutumia upako ni kosa kubwa kumtafuta Yezebeli kwa kutumia upako, Eliya alijaribu kufanya hivyo akashindwa hatimaye akajikuta mwenyewe kwenye wakati mbaya hata akakimbia, sisi tusilirudie kosa hili alilolifanya Nabii Eliya, Mwana wa Mungu nikosa kubwa kukata kumwua Yezebeli kwa kuutegemea upako, Upako utaweza tu kukusaida kuwachinja manabii wa baali kwasabu hapo unakuwa ni ushindani wa madhabahu kwa madhabahu ili ionekane ni ipi yenye nguvu,

YEZEBELI ANAUAWA KWA MAMLAKA YA KIFALME
Kabla ya kupambana na Yezebeli ni lazima utambue kuwa Yezebeli yupo ikulu na anamajeshi nyuma yake sasa ili kumuweza ni lazima na wewe uvae mamlaka ya kifalme hii sasa itakuwa ni vita ya Falme kwa falme, tofauti na ile ya madhabahu kwa madhabahu ambayo Eliya alishinda, kwakuwa yeye ni nabii wa Mungu anayeibeba Madhabahu ya Mungu alipigana vita na manabii wa baali, lakini hii ya Yezebeli ni ya kifame ambayo ilihitaji mfame na ndiyo sababu Yehu aliishinda na kufanikiwa kumwua Yezebeli kwa sababu Yeye alimwndea Yezebeli kwa cheo cha kifalme hakwenda na kofia ya unabii kama Baba yake wa kiroho alivyofanya, kwakuwa angefanya hivyo nayeye angeshindwa maana hii ni kanuni ya Mungu.

Kosa kubwa alilofanya Nabii Eliya kutompaka mtu mafuta ya kifalme, hili lilikuwa ni kosa kubwa ambalo mwanafunzi wake Elisha alilitambua kosa hilo ndiyo sababu Elisha hakumfwata Yezebeli yeye binafsi bali alichokifanya ni kummiminia Yehu mafuta ya kifalme ili akaifanye kazi hiyo,

Mwana wa Mungu je wewe unapambana vita ya namnagani? Je ni ya kimadhabahu yani yakikuhani au ya kifalme Elewa neno hili kamwe usivamie Ufalme kama wewe Unatetea madhabu na kamwe usivamie vita ya madhabahu kama wewe unasimama nafasi ya kifalme maana kwa kufanya hivyo vita itakushinda na mwishowe utaishia kukimbia kama Eliya na wengi leo wameshindwa na kukimbia=1WAFALME 18:17-4O./ 19:1-3./ 2WAFALME 9:1-37.


Na mtumishi Peter Lukuta

Kwa Ushauri Na Maombezi Tuma Masage Kwenye Whtsapp 0767 503054.

YANGU NI HAYO TU

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

One Response to YEZEBELI HAUAWI KWA UPAKO

  1. Yusha says:

    Mafundisho mazuri sana;ila sija yaelewa vizuri,nilikua naomba ufafanuzi;madhabau yanamaanisha nini kwa kanisa,na ufalme unamaana gani pia kwa kanisa.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s