REALLITY

Reality ni ukurasa mpaya ambao utakuwa ukizungumzia matendao makuu ya Mungu katika Kanisa la leo, Ukurasa huu utakuwa ukihoji juu ya miujiza ambayo inafanyika katika kanisa la sasa ya kwamba ni Mungu anayetenda ama ni Shetani. Katika ukurasa huu tutatoa fursa kwa wewe msomaji wetu kutoa mtazamo wako na mawazo yako juu ya mada itakayokuwa ikiendelea.

Leo tunatazama juu ya mtumishi wa Mungu Mch .Josephat Gwajima wa kanisa la Glory of Christ au Ufufuo na Uzima. Mtumishi huyu amekuwa akitumika kwa Ishara na Miujiza ukiwemo ule muujiza mkubwa wa kufufua wafu na kuwarejesha waliochukuliwa misukule, nakumbuka niliwahi kuwaona baadhi ya watu waliokuwa wamechukuliwa misukule na waliokuwa wamekufa wakafufuliwa kwa mkono wa Mtumishi huyu ni kama watu 200 hivi. Gwajima amekuwa msaada mkubwa sana katika kizazi hiki. Lakini Leo tunataka kuuliza juu ya Miujiza ambayo inafanyika katika kanisa hili je ni ya Mungu kweli au ni ya Shetani? Tunaomba utoe mawazo yako juu ya hili na jinsi unavyomfahamu Mch.Gwajima.

ILANI:
Kuhoji huku sio kwamba tunamaana kwamba Gwajima anatumika kwa Shetani.

Advertisements

67 Responses to REALLITY

 1. Ambwene Luhanjo says:

  Jamani ila kusema kweli hata mimi ninawasi wasi sana na huyu mtumishi, mh kwa nini Misukule arudisshe yeye tu? halafu kwa nini hafanyi mikutano mikubwa na kuwataka watu waache maasi (dhambi) kama wanaavyofanya wenzake akina kakobe? Mmh nimeshituka mwenzenu.

  Like

  • Dickson Kamugisha says:

   Wateule wa Yesu tunatakiwa kutafuta macho na masikio ya rohoni maana hii ndiyo
   changamoto kubwa katika nyakati hizi za hatari(ISAYA 42:18-20).
   Kwa sasa idadi kubwa sana ya wateule wa Mungu wamechukuliwa mateka na kugeuzwa
   misukule inayoonekana ndani ya huduma za miujiza ya shetani yaani makanisa ya manabii
   ambayo hayako katika misingi ya AGANO JIPYA(ISAYA 42:22,MATHAYO 24:24,25).

   MWENYE MACHO YA ROHONI HATAZAMI MWILINI BALI ANAZAMA KWENYE
   ULIMWENGU WA ROHO ZILIPOFICHWA SIRI ZOTE ZA MFUMO HUU WA MAMBO.

   Like

 2. makono Mabula says:

  Haha tatizo watu mnaamini kwamba Shetani peke yake ndiye anaweza kufanya miujiza mikubwa, lakini Mungu hawezi! hebu jifikirieni kati ya Mungu na Shetani nani mwenye uweza mkubwa? mwacheni Bwana mtumishi afanye kazi aliyoitiwa na Mola.

  Like

 3. Yuritha Gwamaka says:

  Ila jamani tunamwamini Mungu lakini pia tukumbuke kwamba Yesu alisema nyakati za mwisho watakuja manabii wa uongo watafanya ishara kuuuubwa hata moto watashusha kutoka angani.

  Like

 4. Emmanuel magambo says:

  Kweli kabisa Makono watu hawaamini kama Mungu anaweza ila wanaamini kwamba Shetani ndiye mwenye Nguvu za kufanya miujiza, big up mtu wangu tuko pamoja,

  Like

  • LUCY FRANCIS says:

   nakuunga mkono magol mana watu wanamwamini shetani kuliko Mungu hao hao unawakuta kwa waganga wanapeleka kafara ndugu zao ndo mana wanawapiga vita watumish wa Mungu mana wanajua wataumbuliwa

   Like

 5. Sharon Ibrahim says:

  Nyote mwasema msiyoyajua Tangu lini Nabii akatoka nje ya Israel? si ninyi wakristo hudai hivi leo vipi tena nabii atoke tanzania?

  Like

 6. mama neema says:

  Kusema kweli mimi simjuwi huyu mtumishi namsikia tu watu wakisema sema kwamba anatumia Lagos, sijuwi kama ni kweli, lakini kuna watu ambao kazi yao ni kuwachafua watu wa mungu hili nalo tulijue ndugu zangu. Namshukuru a liyeanzisha hii mada.

  Like

 7. Amos Rurita says:

  Makono Mabula rafiki yangu hivi umesahau kama wakati wa Paulo alikuwepo mtu mchawi jina lake Bar-Yesu aliwavuta watu wengi kwa uchawi wake wakidhani kwamba hufanya kwa mkono wa Mungu, hata Paulo alipomkemea. kama Gwajima anatumia nguvu za Bar-Yesu ipo siku atakapofikiwa na akina Paulo wa siku hizi atakiona cha mtema kuni, na kama yu-amtumikia Mungu katika Roho na kweli thawabu yake ipo.

  Like

 8. David Mgongolwa says:

  Jamani, baada ya kusoma coments nying hapo juu nimegundua wengi hawajawahi kumsikia hata kumwona Mch. Gwajima
  Nikodemu{mmoja wa Farisayo} alipockia watu wanamsema Yesu vibaya yeye aliwambia ‘kwani torati humuhukumu mtu kabla ya kumsikiliza’
  mtu aliyesema Gwajima hana mikutano ya nje namshauri aende kawe akaone Gari la madhabahu kwa ajili ya mikutan
  mmoja amedai kwann arudishe misukule yeye tu ‘huu n upeo mdogo wa maarifa ya neno la Mungu’ kila nabii aliinuriwa kwa nyakati na majira mfan Elia, Elisha, n.K hawakuwa sawa kiutendaji Mwingine aliambiwa aoe kahaba ili atoe unabii!
  Pia mfano sasa Mwingira funguka{efatha}, Kakobe saa ya uponyaj, Rwakatare Faraja , Gwajima saa ya ufufuo na uzima!
  Mungu anasema msiwaguse masihi {wapakwa mafuta} wake! Ni laana kumsema mtumish wa Mungu vibaya mbele ya watu badala ya kuchukua jukumu la kuomba
  Yesu alisema manabii wa uongo watatambulika kwa matunda ya matendo yao {matokeo ya wanayotenda} kufufua wafu c jambo baya wala geni, Yesu alifufua, Paulo na Petro pia! Yesu akasema yeye aniaminiye mimi kazi nizifanyazo naye atafanya naam na kubwa kuliko hizo maana mm naenda kwa baba’
  xo kazi kubwa n zipi ‘Acheni kumfungia Mungu kwenye box}
  Mungu anamtumia Gwajima kama anavyotumia watumishi wake wengi na kama kazi ni ya Mungu itadumu kwa mujibu ya tovuti yao http://www.ufufuonauzimaministries.org huduma imeanza 1994 upo hapo!
  Waumini zaidi ya 60000, ambao ingawa wako viwanjan bado wanafuata
  “uctumie muda mwingi kupinga tulia jifunze then uamue”
  mwisho huwa kwa misukule anasimamia andiko la isaya 42:22 barikiwa!

  Like

  • Anastazia mkumbo says:

   Bwana yesu asifiwe, Asante sana Davie kwa majibu mazuri, mimi pia nilikuwa nataka kusema lakini niliguna kutokana na watu walivyokuwa wakisema, lakini sasa nimefungua kinywa, kwa kweli Gwajima namfahamu japo si sana, nimewahi kwenda kanisani kwake mara kadhaa, sikuona ubaya sana kwake, lakini kunakitu alifundisha kuhusu Nyota, akasema kila mtu ananyota, mimi kwa kweli niliguna kabisa mh, haya si mambo ya akina Shekh Yahaya! alisema kwamba unaweza kukuta mtu ana nyota ya biashara, pia alizidi kusema kwamba wachawi huiba nyota hizo. mimi ndo kabisa nikazidi kuwa na shaka naye kwa kweli Mungu anisaidie, nawaheshimu sana watumishi wa Mungu, hivyo nikitaka kusema Gwajima si mtumishi nasikia kitu kinafanya ndani Mh, na nikitaka kusema kwamba Gwajima ni mtumishi wa Mungu pia nasikia kitu kinaguna Mh. Jamani naomba mniombee tu katika hilo.

   Like

  • hokoli says:

   Hivi huyu gwajima yukoje, mbona hatumjuwi? yuko wapi? kanisa lake linaitwaje?

   Like

  • Amos Rurita says:

   wewe David umesema vizuri, lakini bado mimi nadukuduku, Yesu alisema nyakati za Mwisho watakuja mabii wa uongo wakifanya ishara kubwa, mtawatambua kwa matunda yao. hivi hebu niambie hao mabii wa uongo ni akina nani? na hizo ishara kubwa ni zipi? na hayo matunda yao ni yapi?

   Like

  • james kondo says:

   mimi kwa kweli sisemi kama ni wa shetani au ni wa Mungu, siri hii anaijua yeye yaani Gwajima na Mungu, akiwepo mwanadamu ni yule anayesaidiana naye.

   Like

  • emmanule akuya says:

   David mimi natubu kuanzia sasa, nilisema mabay juu ya masihi wa Bwana naomba unipe namba yake ya simu ili nimwombe msamaha, au nakuomba unisaidie kuniombea msamaha kwake. Ubarikiwe sana David

   Like

   • David Mgongolwa says:

    usiogope kaka Emmanuel, Mungu anafahamu moyo wako kuliko mimi ninavyofahamu ! AMEKUSAMEHE Anasema ‘tusijidanganye kuwa hatuna dhambi na kweli haimo ndani yetu lakini tukiungama na kutubu yeye ni mwaminifu na wa haki hata kutusamehe kabisa’ yeye atarudi wiki ijayo ila kuna namba ya Mchg. msaidizi atakusaidia 0713254210 Barikiwa

    Like

 9. Omar Hussen says:

  Sasa yamewashinda mpka mmeanza kutiliana shaka ninyi kwa ninyi, tunawaambia mwaminini mwenyezi mungu mmoja na mtume , hamtahi mnasema eti Yesu Mungu, wapi basi hata kwenye Bibilia huyo yesu aseme mimi ni Mungu?

  Like

  • Moses Mayila says:

   Rafiki yangu Omar Hussen, Yohana 14:6 Yesu aliombwa na wanafunzi wake kwamba awaonyeshe Mungu yatosha Yesu akajibu Tangu nimekaa nanyi siku zote hizo msinijue, aliyeniona mimi amemwona Mungu. halafu hoja nyingine unatushauri tumwani mwenyezi Mungu na mtume, sisi tunamwamini mwenyezi Mungu ambaye ni Yehova, na mitume wake yaani akina Mathayo,Petro na wengineo. sasa labda utuambie ni Mungu gani huyo tusiyemwamini na mtume wake yupi tusemwamini. Bwana Yesu akusaidie.

   Like

   • David Mgongolwa says:

    akhsante sana Ev Moses , ‘ kwa maana hakuna njia nyingine tuliyopewa wanadamu itupasayo kuokolewa isipo kuwa Yesu’ sijui huyu ametoka wapi na mtume wake jamani!

    Like

   • mosespk says:

    Unajua Davie huyu rafiki yetu ametuhukumu sisi kwa makosa mawili (1) Hatumwamini Mwenyezi Mungu. (2) Hatumwamini Mtume. sasa mimi nimemjibu kwamba rafiki yetu sisi (1) Twamwamini Mwenyezi Mungu (2) Twawaamini Mitume wake wote. kwa majibu hayo nikasema moyoni mwangu labda huyu ndugu yetu anajipya ambalo sisi hatulijuwi jamani, nikamtaka kwa roho safi atuambie huyo mwenyezi Mungu tusiyemwamini ni yupi? na huyo mtume tusiyemwamini ni yupi? jamaa wetu hajanijibu. lakini nimeona hakuna sababu ya kuzunguka sana acha niseme tu wazi. Huyu ndugu yetu katika mwili alikuwa na maana ya Mwenyezi mungu wake yaani ALLAH na Mtume wake yaani MUHAMAD. sasa jamaa yetu sisi hawa wote hatuwaamini kwa sababu zifuatazo: ukisoma qruan 3:90 inasema Ulevi ni kazi ya shetani, kisha ukisoma 47:15 ALLAH ameandaa mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao. Je bado hujajua ya kwamba huyu ndiye Shetani mwenyewe? pili hatumwamini mtume wake kwa sababu hii: Ukisoma katika kitabu cha MKWELI MWANIFU kinasema, MUHAMAD alikabwa na mashetani kule kwenye majabali, na hata aliporudi kwa mkewe nyumbani alikiri kwa kinywa chake akisema “Najihofia nafsi yangu nimechezewa na mashetani” Mkewe akamwambia usiseme hivyo, shetani hawezi kumchezea mtu kama wewe unafanya hivi na hivi, mh mimi naona umepata UTUME, Kisha Mkewe akaenda kwa Padre mmoja hivi akamweleza yaliyompata mumewe yule padre naye akasema, ah UTUME huo, kisha mkewe akarudi nyumbani kwa mumewe. toka siku hiyo MUHAMAD akaanza kujitangaza kwamba yeye ni mtume wa mwenyezi Mungu. Jamani hivi kila mwenye akili ajiulize mtu aliyekuwa amekabwa na mashetani anasema ati alipewa utume katika huko kukabwa, basi ni dhahiri kwamba alipewa utume wa kishetani. Mbarikiwe mwenye challenge karibu.

    Ev.Moses Mayila

    Like

   • David Mgongolwa says:

    kwa kweli nimeipenda hiyo na sina nyongeza maana hata mimi nimeelimika lol!
    kumbe hana lolote kapewa utume na mkewe lol! akhsante

    Like

 10. emmanuel mabuga says:

  Sisi tujadili habari za Gwajima, huyo anayeleta habari za mtume wake ametoka wapi huyo?

  Like

 11. ysin thabith says:

  hakuna lililojificha ambalo halitafunuliwa, kama gwajima kajivika ngozi ya mbuzi kumbe mbwa mwitu atajulikana tu, na kama Bwana amempaka mafuta ili amtumikie itajulikana. zaidi sana tuzidi kumuuliza mungu juu ya hili.

  Like

 12. abimeleki faaustin says:

  kaka david hongerea sana kwa ufafanuzi mzuri mimi naomba unielekeze hilo kanisa lilipo, kwa hapa mbeya. asantte sana.

  Like

  • David Mgongolwa says:

   kusema kweli bado halijafungua tawi mbeya , ila kiwanja kimepatikana kwahiyo hivi karibuni litafunguliwa huko, Barikiwa kaka Abimaleki

   Like

  • greuben76 says:

   Mtawatambua kwa matunda yao, matunda ya Gwajima yako wazi, kama anaenenda sawa na neno la Mungu Ni saws. ILA napata wasiwasi katika Hilo.

   Like

 13. David Mgongolwa says:

  Mbarikiwe wote mliochangia na kuniuliza maswali
  labda nianze na HOKOLI aliye uliza MCH. GWAJIMA YUKOJE, huyu ni mchungaji kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima lenye makao yake makuu Kawe {Tanganyika peakers} ambalo awali lilikuwa Ubungo. maarufu kama ufufuo na uzima , kanisa la kiroho
  Anastazia …anauliza kwa habari ya nyota………ni kweli niliwahi kusikia somo la nyota kutoka kwa mch. Gwajima, na katika somo hilo alitumia maandiko mengi ili aeleweke kimsingi alisema “nyota ni tafsiri ya uwezo aliopewa mtu na Mungu ili umsaidie kuishi kwa mafanikio inaweza ikawa kipaji , michezon.k, ” akaendelea kwa kutoa mfano wa ” Yesu alipozaliwa nyota yake ilionekana mashariki iking’aa na walioifuata ni mamajusi{magicians,wasoma nyota,} kwann alifundisha nyota kwasababu watu wengi wameibiwa vipawana shetani coz wachawi huwa wanaiba na kuwauzia wengine either viongozi n.k {zaidi CDs zinapatikana.
  AMOSI Rulita anauliza je manabii wa uongo anaosema YESU tutawajuaje Yesu alisema “watakuja manabii wa uongo nanyi mtawajua kwa matunda ya matendo yao!” akimaanisha kwa yale wanotenda , ndo maana kuna manabii sikuizi ukitaka mtoto anataka ulale kwa madai Mungu amesema! sikatai kuwa hawapo wapo tena wengi, “na ndiyo maana agano la kale Mungu akasema mtu atakayetoa unabii alafu lisitimie mtajua kwamba sikumtuma”
  matendo ni jinsi maisha yao je ni ya kumcha Mungu au anatenda uovu ingawa ni vigumu kutambua lakini ndo njia ya kuwatambua!
  Nirudi kwwenye mada wengi wamesema hawajawahi hata kumuona mi nawashauri watembelee kanisani au ukishindwa nunua hata kanda umsikilize akifundisha!!!!
  watu wengi huwa wanatarajia Mungu anatumia watu ambao wewe unadhani wanafaa lakini Mungu hutumia watu usiowadhania(wanyonge) huduma hii ilianza 1994 hadi leo ipo….. kitu kama si cha Mungu akiwezi dumu!! Mungu anafungua wengi na ni kanisa lenye wachungaji wengi wanahudumia watu masaa 24, kuna mikesha kila siku je bado ni shetani!
  Mchg. Gwajima aliwahi funga akikaa pale kanisani kwa kunywa maji tu siku 40, na aliondoka kwa kubebwa! waliokuwepo watakubaliana na mama! ukiona huduma imesimama kuna mahali imetokea ………aliokoka baada ya kuugua miaka 6 mfululizo
  Kabla hujafuata watu wengine kumsema vibaya ni muhimu kujua kama ni mtumishi wa kweli wa MUNGU aliyelipa gharama basi unachuma laana kwenye maisha yako
  bora utulie ujifunze then uamue kwa AMANI YA KRISTO ILIYO NDANI YAKO!!!
  BWANA AWABARIKI SANA!!!!!!

  Like

  • Joseph says:

   Ivi twende mbele na kurudi nyuma. Ivi PORNOGRAPHY ni nini???

   Like

  • Joseph says:

   Nnna swali, Ila ili kuepuka kunichanganya kwa sababu nia yangu nielewe na niweze kuwaeleza kwa ufasaha watu watakaoniuliza, naomba swali hili alijibu mtu ambaye ameokoka kweli na ana uhakika 100% ameokoka, na ana akili timamu. Aidha nina maswali meeengi sana nataka kupata kujua, lakini ngoja nianze na hil: PORNOGRAPHY NI NINI????

   Like

  • AMOS RULITA says:

   Jamani naomba Mungu anisamehe, mimi kwa kwli nilikuwa simwamini Gwajima, ilibidi jumapili hii niende kanisani kwake, lakini bahati mbay sikumkuta, lakini jinsi nilivyokuta ibada ikifanyika sijaona kasoro kwa kweli wanaombea kwa jina la Yesu. yaani hata mimi ilibidi nipite pale mbele waniombee. lakini bado ninadukuduku kidogo mpaka nimwone yeye akihubiri ndipo nitasema kweli katoka kwa Mungu, lakini nilivyomkuta msaidizi wake akihubiri oh alihubiri kweli yote iliyotoka kwa Bwana. Jamani naomba mnisaidie kuniombea David niombee sana rafiki yangu, mimi simkatai mtumishi huyu kwania mbaya bali ninamsukumo unaotoka moyoni unaonifanya nisimwamini, jamani mnisaidie.

   Like

   • David Mgongolwa says:

    nimependa pale ulipochukua jukumu la kwenda kanisani kwake! na ulichokiona !! nimependa hapo
    na kama nilivyosikia unatamani umune akiwa anahubili nayo sahii, kwasababu anarudi jumapili kutoka japan alikokuwepo takribani mwezi mzima, pia baadhi nya mahubuli yake yanapatikana YOUTUBE , NA kwa kuwa ni vizuri kuombeana kwa kweli!
    nami nitakuombea kwa hilo, kwasababu MUNGU analipenda hilo! nakusihi pia muulize Mungu kuhusu hili pia

    Like

 14. Joseph says:

  Ivi kabla hatujaenda mbali. Watu wanasema na kuhubiri pornography. ivi PORNOGRAPHY ni nini?

  Like

  • mosespk says:

   Joseph Bwana Yesu apewe sifa, napenda kukusaidia tafsiri ya swali lako. Neno Pornography linamaana ya (picha, filamu au michoro) ambayo haina faida zaidi ya kumsababisha mtu kuwaka tamaa ya mwili. nadhani hadi hapa utakuwa umeelewa rafiki yangu.

   Like

 15. Hokoli says:

  Davidi asante sana, unafafanua kwa upole kweli, hata mimi nimeanza kukubali kwa mbali

  Like

 16. Rominda Chonya says:

  Mimi nilikuwa mstari wa mbele kumpinga Gwajima, lakini sasa duh, naomba tusiwahukumu watu kama hawa, kama ni wa uongo watajuana wao na Mungu, mimi kuanzia leo namwamini Gwajima kwa Roho yangu yote, kama si wa kweli nitamuuliza siku hiyo, kwamba “Mwenzetu kumbe ulikuwa unatupiga changa lamcho ukisema tuko pamoja kumbe uko upande wa adui?” lakini kuanzia leo sitasema neno baya tena juu yake, nisije kulaaniwa.

  Like

 17. Bwana Yesu asifiwe, tuweni makini tunapoongelea watumishi wa Mungu. Kama hauna uhakika na kitu ni heri unyamaze kimya! La sivyo tutapigwa ukoma. Eleweni kitu kimoja kwamba watumishi wote kuna jinsi walivyoitwa na Mungu, kila mmoja ana agano na Mungu wake na pia kila mmoja kwa nafasi yake atatoa matunda ya kazi yake hivyo basi, Mungu anachokiona na kukiheshimu ni mafuta aliyowapaka watumishi wa Mungu!

  Like

 18. mosespk says:

  ASANTENI SANA KWA WOTE MLIOCHANGIA MJADALA HUU BWANA AWASAIDIE SANA, KWA UPANDE WETU NASI TUNAPENDA KUTOA KAULI YETU JUU YA MCH.GWAJIMA. NI KWAMBA SISI TUNAMUAMINI GWAJIMA, TUMEMFUATILIA KWA MUDA MREFU SANA KUTAKA KUJUA YAMSEMWAYO NI KWELI AU UONGO. LAKINI TUMEGUNDUA KWAMBA GWAJIMA NI MTUMISHI MWEMA WA MUNGU. BIBLIA ILIPOSEMA MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO, HAPA YESU ALIMAANISHA MAFUNDISHO YAO, SASA TUMEPITA SANA KATIKA MAFUNDISHO YA GWAJIMA ILI KUONA KAMA NI YA KISHETANI KWA KWELI HATUJAONA KITU KAMA HICHO, SISI NI WA KWELI HUWA TUNASEMA KWELI HATUZUNGUKI. JAPOKUWA KUNA BAADHI YA MAFUNDISHO YAKE KIDOGO YANALETA UTATA LAKINI SI KWAMBA AMAKEWA MTUMISHI WA SHETANI. BWANA AWABARIKI NYOTE.

  NEW HOPE MINISTRY TEAM.

  Like

 19. Kashmir bashir says:

  Utukufu ambao hawana imani na mchungaji Gwajima nawapa pole

  Like

 20. julieth says:

  naweza kusema kwamba hili ni jukwaa zuri sana nimelipenda kuwepo hapa, nimefurahi kusikia na kuona watu wenye uelewa kama David na watu wanaoshaurika kama hokoli na Chonya. mimi nami nataka kusa walau kidogo. haya mambo huwa ni siri ya mtu ambayo inakuwa moyoni mwake, sasa wale wanaosema huyu anatumia mashetani wamejuaje? hebu naomba mniambie nyinyi mnaodai Mchungaji anatumia ushirikina mmeptaje kujua?

  Like

 21. Abby Grancia Rutta says:

  Ambwene kaka yangu!! Mungu umtumia mtu kwa jinsi anvyojitoa kwake ukimwekea limitation ucdhani kwamba ataenda beyond ur vision,Gwajima ameamua kumbeba Yesu jinsi alivyo na ndo maana anatumika kwa ilo, na pia kila mtumishi ameitwa kwa namna yake kuna walioitwa kufariji, wengine wameitwa kufungua vifungo na mengine yote hayo ni maono yao lakini pia kwa kaka hapo juu alosema Gwajima hakemei DHAMBI naomba nimuulize je aklishawahi kuudhuria seminar zake nakusikia kwamba hafanyi kitu icho? kiukweli yule baba kwanza anaichukia dhambi na kumchukia shetani kuliko tujuavyo kwasababu shetani ndo mwanzilishi wa dhambi …mbona Yesu alimfufua Lazaro je biblia hajaisema kwamba na makubwa zaidi ya hayo tutatenda.barikiwa

  Like

  • David Mgongolwa says:

   AMEN, Abby, watu wanashau kuwa Mungu akikuita anakupa na jukumu , na hakuna wito kama hakuna jukumu, alimwita Musa jukumu watoe isrel kutoka utumwani Misri, Mfalme saul angamiza Amaleki, Daud angamiza wafilisti, wote walikuwa na wito tofauti Suleimani Jenga HEKALU N.K,
   ” Yesu alisema asikinyume nasi yu upande wetu” alisema akijua haya yatatokea
   asante Abby may God bless you

   Like

 22. Jamar Dively says:

  I am a democrat, but I didnt vote for Obama- Im not that CRAZY!!!!!!!!

  Like

 23. Glenn Flach says:

  The one game that sticks in my memory is vs Arsenal 1973 (I think). We were 0-1 down with 20 minutes left and Jinky was sub (only one allowed then!) as he had been out for weeks with the re-occurring knee cartilage problem.

  Like

 24. I just added your RSS Feed on my RSS reader, it is so nice to read your blog

  Like

 25. My spouse and I absolutely love your blog and find nearly all of your post’s to be exactly I’m looking for. Does one offer guest writers to write content for you? I wouldn’t mind creating a post or elaborating on a few of the subjects you write with regards to here. Again, awesome web log!

  Like

 26. dart cases says:

  1st Place SHEARER2nd Place Andy Cole3rd Place Gary Speed/Rob Lee

  Like

 27. Praise says:

  Inasikitisha sana, kutokuamini kwa wanaojiita wakristo wa Tanzania! Inasikitisha sana, Mungu wenu ni mkuu sana alifanya mambo makubwa kuliko mnayoyaona na kusikia kwa Gwajima. Kwa nini kumhuzunisha Roho Mtakatifu? Kila siku mnaliombea Taifa lenu Mungu akianza kuwajibu vinywa vyenu vinajaa makufuru; Mimi najuta kwa kusoma mawazo yenu haya na kamwe sitarudia kusoma post zenu tena! Im sorry for this

  Like

 28. Yusha says:

  Hatari

  Like

 29. Yusha says:

  Wameishaka pata dhawabu yao.

  Like

 30. nemes asenga says:

  ki ukwel huyo mtumishi wa Mungu me simfahau jaman naomba mnipe video zake na more data if possible

  Like

 31. Pastor Oswald says:

  Hata Yesu mwenyewe alisema kazi nizifanyazo mtazifanya na zaidi ya hizo.

  Like

 32. Joaseph Timothy says:

  Nahitaji kuwasaidia sana kuhusu kitu ambabcho kimekua kinawasumbua sana kuhusu kumtambua mtumishi wa Mungu.maana nimegundua kumbe ni kweli kabisa kama mtu anaweza kuanzisha huduma fulani ya kiroho na kisha akawa na miujiza mingi basi ni dhahiri kwamba mtu huyo anauwezekano wa kuteka watu wengi sana yamkini hata wateule hata kama sio mtumishi halali.sina maana ya kwamba Gwajima sio mtumishi! hapana msinielewe hivyo maana hata Gwajima mwenyewe mi simfahamu, japo nimeokoka na kiukweli nahitaji kuurithi uzima wa millele.Kama kuna mtu anahita kufahamu namna ya kuwatambua watumishi tafadhari tuwasiliane kupitia: josephtimothm@gmail.com nitampa angalao maelezo juu ya hilo

  Like

 33. joshua john says:

  ni vigumu kuthibitisha kuwa mch Gwajima, kwamba anatumia nguvu za giza,kwan ktk maandiko matakatifu hususan kitabu cha mathayo 28:19-20,marko1:38-41,10:34-38 vinaonesha jinsi mungu anavyotukabidhi mamlaka ya kulitangaza neno lake popote pale duniani

  Like

 34. joshua john says:

  wanaohitaji ushaur zaidi pamoja na maswali wasiliana nami:mzaliwaathuman@gmail.com kwa msaada zaid kiiman

  Like

 35. erastus says:

  Huyo ni mch.josphat ngwajima anatumiwa na Mungu kwa jia hiyo.
  swali: 1. wewe mnafanya niniiiiiii??????
  2. unaweza kufanya kitu pia uhishagaze dunia????
  3. Yote anayoyafanya si yameadikwa kwa bibilia???????!
  Kama wafu wanafufuka kwa kulitia jina la Yesu,..JE ? wale mnabisha mnataka kusema kwa jina la shetani pia watafufuka?????

  from kenya.

  Like

 36. William Nathaniel says:

  mlitaka shetani ndo afufue wafu…wapumbavu

  mnahoji utendaji wa Mungu kwa mapokeo yenu ya kiibilisi

  sasa nani afanye zaidi ya alofanya Yesu?!

  Like

  • greuben76 says:

   Acha upumbavu wewe! Ni nani aliyemfufua ambaye ulikuwa unamfahamu? Kama anaweza Ni maiti ngapi amaletewa akazifufua hapo kanisani kwake? Watu mnaangamia kwa kukosa marifa.

   Like

 37. Athanase mkoma says:

  Hébreux 6:1-3

  Jamani naomba ni changie japo kiswaili siwezi vizuri (DRC)
  kuhubiri dhambi kila siku si kigezo cha kuwa sahihi, nakanisa likihubiriwa dhambi kila leo hilo kanisa linamatatizo ya kutobadilika ama kukua kiRoho na halito enda popote maana mafundisha ya toba ni mafundisha ya mwazo ya maneno ya Mungu(msingi) hayo yatahubiriwa kama Bwana akiongoza, soma andiko hapo juu,
  Palipo na utii wa sheria, sheria haizungumziwi kila siku,
  Ukiona kanisa lako watu hawa badiliki bado niwenye dhambi kila siku BASI HUBIRI DHAMBI HADI WATAKAPO BADILIKA. Ukisha umaliza msingi huu ndo uendelee na mahubiri mengine

  Nihaibu kusikia kila siku kanisani hacha dhambi hacha dhambi kwani hamjabadilika ?bado wenye dhambi tu ?

  Somo la dhambi nila siku chache na mtu akishabadilika yanaendelea mafundisho mengine, mtu akijikwaa ataonywa

  Mbarikiwe wapendwa.

  Like

 38. Athanase mkoma says:

  Hivi tunalielewa neno la Yesu asemapo wengi watakuja kwangozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu,

  -Nikwamaba watalihubiri Neno la Mungu kiusahihi (kondoo) lenye sura kristo na ukimtafuta kwenye Bibilia utampata hayuko nje ya maandiko, lakini kumbuka andiko la uwa bali Roho utia uzima
  – Jambo la msingi: ni viema kufahamu si usahihi wa mafundisho tu (ngozi ya kondoo) bali tafuta kujua ni roho hipi inayotenda kazi nyuma ya hayo mafundisho ?(ni Roho wa kristo au mbwa mwitu ?)
  – Kinacho mbadirisha mtu si mafundisho tu bali ni Roho mtakatifu aliye ndani ya mafundisho, hapo ndipo penye siri wana wa Mungu, neno nikama chambo kwenye ndoani na samaki anapo kipenda hichochakula basi kitakacho mnasa si chambo (Neno =kondoo)bali ndoani (Roho mtakatifu /au roho mbwa mwitu)

  Mtu hatakama atahubiri dhambi sana watu hawewezi kubadirika ikiwa roho aliye nyuma ya mafundisho si wa Mungu(mbwa mwitu) maana huyo roho (mbwa mwitu) ndiye watakeye mmeza watazidi kufanywa kuwa wana wa shetani.
  Ukiliamini Neno lisilo na Roho mtakatifu hata kama ninzuri kibibilia haliwezi kukubaririsha
  -YESU alisema msiende kwanza kuhubiri hadi mtakapo pokea nguvu akisha kuwalilia Roho mtakatifu.
  -Ndio maana Hata waganga na wachawi wanaweza kuitumia bibilia na kuhubiri neno nzuri( kondoo)hadi ukasema amen, lakini roho utakayo meza ni roho mbwa mwitu
  -Usijindanganye na kusema mchungaji uyu ndio wa kweli kisa ana kemea dhambi sana bali angalia matunda yani matokeo ya mafundisho kwa wanaofundishwa, hayo ndo matunda,
  Paulo anasema niyi ni Muhubiri wa utumishi wangu.

  Ninayo mengi wapendwa ukitaka zaidi tuwasiliane +255746702351

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s