TULIKOTOKA


Tulikotoka ni ukurasa mpya ambao utakuwa unazungumzia maisha ya watumishi wa Mungu katika Utumishi wao, Jinsi walivyoitwa na kuanza Utumishi hadi hapa walipo leo. Leo tutammurika mtumishi wa Mungu Askofu Moses Kulola.
Moses alikuwa ni Engineer wa ujenzi ambapo Mungu alimwita na kulazimika kuachana na mambo ya ujenzi na kuanza kumtumikia Mungu. Moses aliacha kazi na kwenda mlimani kufunga na kusali kwa muda wa siku kadhaa, alipokuwa akiondoka nyumbani kwake alimuaga mkewe akamwambia kama nisiporudi basi ujue nimekufa. huko mlimani alijaribiwa na Ibirisi ambapo usiku wa manane aliona watu wakiwa wamevaa mavazi meusi akawauliza “Nyinyi ni akina nani?” wakamuuliza na wewe ni nani? akasema mimi ni mtumishi wa Mungu aliye hai. mara wale watu wakaenda zao. Mvua zilimnyeshea Moses, baridi nalo lilimpiga, usiku wa manane akiwa amebeba Biblia yake kwapani amenyeshewa mvua baridi linampiga anatetemeka, kalala juu ya mwamba mara akashituka na kuona yuko chini ya uvungu wa Mnyama mkubwa sana, Moses akamkemea yule mnyama kwa Jina la Yesu na mnyama yule akaenda zake. Ilipofika muda flani Usiku alisikia Sauti ikimwita kwa jina “MOSES” na hii sauti haikuwa ya mwanamke wala mwanaume sauti ile ikasema kwake “Tazama nimekufanya kuwa mtumishi wangu ukaniletee kondoo” Sauti hii ilikuwa ni ya Mungu Mwenyewe. Ndipo sasa Moses alipotoka mlimani na kurudi nyumbani kwake na baada ya hapo alianza kuhubiri habari za yesu na ishara na Miujiza zikaambatana naye, Moses akawa Moses aliitikisa Africa sana. Hapakuwa na mtu aliyeitikisa Africa kipindi hicho kama Moses Kulola. Bwana asimuache mtumishi huyu katika nyakati zake hizi za mwisho. Kusema kweli hesabu ya Siku za mtumishi huyu kuwa naye kwa sasa si nyingi tena, maana hata yeye alishawahi kutangaza katika kongamano moja lililofanyika 2005 kama sikosei akasema akizitazama siku zake zimebaki kidogo. Bwana amshike mkono mtumishi wake katika Jina la YEsu. Amen

25 Responses to TULIKOTOKA

  1. Hermany Joseph says:

    Ama kweli mtumishi huyu ametoka mbali, huyu kweli aliokoka kumaanisha na aliitwa kutumika na Mungu mwenyewe tofauti na watumishi ambao hujiingiza katika utumishi ili kwamba wapate fedha. Bwana amlinde Kulola wetu.

    Like

  2. Oretha Batta says:

    I simply want to tell you that I am just very new to weblog and absolutely loved your web site. Probably I’m going to bookmark your blog post . You certainly come with incredible posts. Kudos for sharing with us your blog site.

    Like

  3. I just want to mention I’m beginner to blogs and really savored this website. Very likely I’m going to bookmark your website . You really have outstanding writings. Kudos for sharing with us your web page.

    Like

  4. Hull needs a manager, will they try to grab our CH?

    Like

  5. Rhett Riddel says:

    Now lets think about what other teams with this problem have been doing. Lets take Jacksonville, for example. Losing two of their lineman without having adequate replacements have 1) taken away the effectiveness of Fred Taylor and 2) meant that theyve had to use MJD on short passes out in the flat. Mewelde has similar skills to MJD (though possibly not the talent), and his best numbers have come in the short passing game.

    Like

  6. I simply want to say I’m beginner to blogging and absolutely liked you’re website. Likely I’m going to bookmark your website . You certainly come with exceptional stories. Thank you for sharing your website.

    Like

  7. Have you ever thought about including a little bit more than just your articles? I mean, what you say is important and everything. However think about if you added some great images or video clips to give your posts more, “pop”! Your content is excellent but with images and clips, this blog could certainly be one of the greatest in its field. Wonderful blog!

    Like

  8. Really excellent visual appeal on this internet site , I’d value it 10 10.

    Like

  9. Definitely, what a magnificent blog and enlightening posts, I will bookmark your site.Have an awsome day!

    Like

  10. orbi says:

    Ni kweli Mzee Kulola ana histori ndefu katika Kuihubiri Injili Tanzania….hilo halina Ubishi…lakini ukitaka kuiandika historia pasipo kuipindisha ana mchango mkubwa pia katika kulipasua Kanisa la Assemblies of God….huo ni ukweli usiokimbilika……nilikuwepo Kanisani nikiwa kijana mdogo alitoka kuokoka Tabora wakati machafuko ya Kanisa la Assembilies of God….nilikuwepo Mahakamani nikifuatilizia kesi iliyotoa maamuzi ya kulipasua Kanisa la Assembilies of God……nilipata uchungu mno kuona Kulola akiongozwa kujitetea chini ya Mwanasheria Muislamu mwenye siasa kali (Nadhani sasa ni Marehemu- Kwikima) akiongoza jopo la Utetezi la Kulola……..Si kwamba upande wa pili haukuwa na makosa la hasha!……..Kwangu Mimi Mzee Kulola alinipa somo kubwa….kutofuata viongozi kama muhiumili wangu wa Imani…….

    Like

    • tunashukuru sana Orbi kwa mchango wako katika mada hii. Bwana akubariki sana.

      Like

      • orbi says:

        Nashukuru ndugu zangu wa Hope Ministry…….Kwangu mimi naamini Tanzania tunahitaji t

        Wapendwa wana New Hope Ministry……..naamini kila anayeijua historia ya Tanzania Enzi za miaka ya 80 kila Mtu anakiri Uwepo wa Mungu ulikuwa juu ya Taifa…..Injili ilikuwa na Ujumbe Mfupi; Kutubu, Kuacha Dhambi,Kutembea Maisha Matakatifu, Na kumsubiri Yesu kurudi kulichukua Kanisa! Hatukuwa na Injili za Mafanikio! Hatukuwa na Matamasha ya Muziki! Hatukuwa na TV! hatukuwa na waumini wengi wenye mali na cheo…….hatukuwa na majengo ya hadhi….au waumini wenye magari….!Na kila Muumini wa Kristo alijaribu mno kujitofautisha na DUNIA…..

        Lakini kwa kuwa tuna na Njaa na Kiu ya Uamsho wa Wakati ule ni lazima pia kujifunza wapi Kanisa la Mungu lilikwenda Kombo kipindi ……Naamini kwamba Tumaini au Imani ya Muumini ni lazima ijengwe juu ya Kristo……Kristo tu na Neno lake…..makosa yaliyofanyika miaka ya 80 ilikuwa ni Imani ya Waumini kuanza kujengwa juu ya Watu……! Kanisa na waumini kusahau kuwa miujiza si kilele cha Imani……..Miujiza ni sehemu tu ya Imani Yetu…na Mtenda Muujiza ni Mungu sio Mtu……..Waumini wa miaka ya 80 wakaanza kuwatukuza akina Kulola/Lazaro na viongozi wakashindwa kutambua kuwa Kanisa si mali yao…….na matokeo yake tuliyaona……..

        Naamini kanisa la Tanzania bado halikujifunza katika hilo…..Hebu angalia leo imani za Wakristo wengi zilivyojengeka juu ya Mitume/Manabii/Watenda Miujiza! Biblia inatufundisha wazi kuwaheshimu wanaotufundisha Maneno ya Mungu…Lakini kuwaheshimu na kuwaenzi huko kuwe katika wigo wa maneno ya Mungu………tu!

        Hivyo licha ya Kumuenzi Mzee Kulola….ambaye tunaamini alifanya kwa sehemu kazi yake….lakini kama binadamu aliyevaa mwili wa nyama alifanya makosa mengi pia……..Kanisa la Assembilies of God lilijengeka katika zamu yake……na vile vile lilipasuka katika zamu yake pia…….Ni Mungu mwenyewe anaweza kufanya tathimi ya halisi ya Kiroho…….Lakini kwetu sisi ni kujifunza kutoka katika kipindi kile, Ili kama Mungu ataamua kuitembelea tena Tanzania na kutuinulia Mtu wake wa kulirejesha taifa hili kwa Mungu tuweze kumuombea….Kumsaidia……sio kumwabudu……na kumwinua…….tukitambua kwamba ni Mungu tu amependa kumtumia kwa makusudi yake yoyote atakaye amua kutuinulia tena …na wala sio Utakatifu….au Utauwa wa mtu huyo…….Naamini Kabisa Mungu ataikumbuka tena Tanzania…na kutuletea Uamsho…….Na kama hatupendi kujifunza kutoka katika shule ya Historia….tunaweza kurudia makosa yale yale….Mbarikiwe na tuzidi kuombea Uamsho wa taifa letu!

        Like

      • Asante sana Orbi, lakini mimi wakati mwingine nadhani kwamba yawezekana ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa Assemblies of God kugawanyika, ili Moses na Lazaro waweze kutumika katika wigo mkubwa! hii ilishatokea hata kwa Mitume, Mungu aliwaagiza wahubiri Injili Duniani pote lakini Mitume waliafikiana kutotawanyika, Mungu akatoa kibali Stephano auawe ili mitume watawanyike, stephano akapigwa mawe hata kufa na mitume wakatawanyika kila mtu njia yake. mimi nafikiri Mungu aliazimia Kulola aachane na Lazaro ili lizaliwe kanisa jingine ndipo likazaliwa TAG. mimi huu ni mtazamo wangu.

        Ev.Moses Mayila

        Like

      • orbi says:

        Mwinjilisti Mayila,

        Mtazamo wangu ni kwamba Mungu anaweza kugeuza jambo lolote lile hata kama likifanyika kwa ubaya kuyafanya Makusudi yake……hapo ndio tunaona Shetani hana uwezo wa Jambo lolote…Na tumeona hivi katika Biblia Nzima……..!

        Siamini Mungu anaweza kutungombanisha ili kufikisha kusudi lake….that will be a bad theology…….kinyume na maneno yake…!Kanisa la kwanza lilitawanyika….Mitume waliuawa…….! Lakini ilikuwa ni vita Nje ya Kanisa sio ndani ya Kanisa….! Hata matenganano ya Paulo na wenzake kuhusu Marko katika safari ya kwanza ya umissionary wa Paulo hayakuligawa kanisa……! Umoja wa Waumini unajaribu kuhifadhiwa kwa gharama yoyote ile……! Sisi ni mwili mmoja wa Kristo……! Hii ndio Imani ya Agano Jipya……!

        Kwangu mimi mgawanyo wa Kanisa ulikuwa kushindwa kwetu kuuishi kama Neno la Mungu linavyotufundisha….na wala haukuwa Mpango wa Mungu…….Faraka…Magomvi….Kamwe si sehemu ya Tunda la Roho…….BALI MUNGU KWA NEEMA YAKE TU ALITUREHEMU HATA KUTOKEA MAKANISA MAWILI…….Na kwa vile sisi ni binadamu hatuna uwezo wa kuangalia yale ambayo hayakutokea…..Je kama Lazaro na Kulola wangeliweza kuyatengeneza matatizo ya kanisa, Je Kanisa lingekuwa wapi leo? Kama kwa kumkosea Mungu tunadai Injili iliweza kusogea mbele kwa kuzaa makanisa mawili…Je kwa kumtukuza Mungu kwa Kuufuata mpango wa Mungu wa kushika maneno yake ……kupendana…Kusameheana……kuchukuliana Kungelifikisha Wapi kanisa?..

        Like

      • Ni kweli Orbi uyasemayo ni kweli kabisa Mungu hawezi kuruhusu ugomvi ndani ya kanisa, lakini kwa matokeo ugomvi wa kulola na Lazaro jibu lake linahitaji utafiti wa ki-theology. Mimi siamini moja kwa moja kwamba Mungu alihusika wala siamini moja kwa moja kwamba shetani alihusika. ila bado nafanya utafiti katika kuyagundua mambo haya. kwa maana angelikuwa shetani matokeo yake yangekuwa mabaya sana, lakini pia kama angelikuwa Mungu ugomvi katika kanisa usingetokea.

        Like

    • Boniface Faustine says:

      Shalom wapendwa ktk BWANA YESU.
      Ndugu zangu ifike wakati wakumuelewa MUNGU kibinafsi nje ya hapo tutakuwa ni watu wakuyumbishwa na maneno ya watu,ikiwa MUNGU anajibu kwa nini tusimtafute yeye ili akueleze ukweli kuhusu watumishi wake..mbona waisraeli walipoweka mashaka juu ya utumishi wa MUSA kwamba kwa nini mungu aseme na yeye tu?je unajua nini kilitokea??tusome neno jamani..Daudi aliogopa kumjudge sauli alisema huyu ni mtumishi wa bwana akashindwa kumuuwa lakini leo hii tumekuwa watu wakunyosha vidole juu ya watumishi,,jililie mwenyewe. Zaidi ya yote ktk bonde la kukata maneno itakuwa ni mwisho itajulikana nani kondoo na yupi ni mbuzi?
      Barikiwa

      Like

    • kwikima Abdulbasit says:

      Kijana mzee wangu bado mzima tafadhali ustumie lugha iyo tena

      Like

  11. Ukwel bwana awe na m2mish wak DR MOSES KULOLA ili amalize salama kwan ndio jicho la EAGT dunian pia MUNGU alaze MCHUNGAJI wangu BISHOP VICENT MWANANDENJE-MAKANYAGIO EAGT-MPANDA MJIN
    JOBS 01:01-
    Bwan alitoa bwana ametwaa

    Like

  12. Justine N.N says:

    Real nimebarikiwa na comment zote, japo nisemacho ni hiki;swala la kumjua Mungu na utendaji wake ni pana sana, thats why wana wa Yakobo walipoenda Misri wakati wa njaa walimuogopa Yusufu ndugu yao kwa vile walivyomtenda, ona alivyowajibu kwa muono mkubwa zaidi kuwa ”kama ninyi mlikusudia maovu bali Mungu alikusudia mema katika maovu yale ili ipate kutokea Mungu kuokoa taifa lake kama hivi leo, kimusingi hata manabii ukitafuta madhaifu yao utayaona, way foward simama kwa zamu yako ukiwa mwenye kujifunza kuepuka makosa ya hao waliotangulia kuiga ushindi nwao.

    Mbalikiwe watu

    July 2012

    Like

  13. Oh let me say R I P Our fathen you have perfomed a lot of goods

    Like

  14. special eyes says:

    mbarikiwe sana watu wa mungu kwa mitazamo yenu lakini leo nakuja na mtazamo mpya kwamba KULOLA amemaliza kazi na sisi je

    Like

  15. Nenda Moses, nenda, tunahuzuni sana lakini nenda, mana imempendeza Bwana uende kwake. nenda mtumishi, na uso wa bwana uende na wewe. nami nazichuchumalia neema za Bwana ili nikuone tena paradiso……….

    Ev.moses mayila – New hope ministry (NHM)

    Like

  16. Bwana apewe Sifa, nimebarikiwa sana na hii habari kuhusu huyu mtumishi wa Mungu

    Like

Leave a comment