DAWA YA MATATIZO YOTE NI YESU

Yesu alisema “Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumuzisha, jitieni nira yangu mkajifunze kwangu maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu, kwa maana nira niwapayo mimi ni laini na mzigo wangu ni mwepesi” Mathayo 11:28-30.
Kwa kawaida kuna watu ambao wanasumbuka na mzigo lakini kwa bahati mbaya hawajuwi kama ni mizigo kwao, na wala hawajuwi ni wapi ta kuitua, kuna magonjwa makubwa yasiyotibika, matizo ya kifamilia,kiuchumi,kielimu n.k. Yote haya ni mizigo ambayo Yesu aliimanisha katika kifungu hiki, lakini yeye anasema uende kwake atakupumuzisha na wewe utakuwa raha katika nafsi yako.
Watu wengi Duniani wamejeribu kutafuta namna ya kujinasua na matatizo walinayo lakini imeshindikana kutokana na uzito wa matatizo hayo, lakini leo ninakutangazia namna ya kujinasua, haijalishi umeteseka kwa Muda mrefu, Yuko Yesu leo anakwenda kukupumzisha, yeye anasema nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi, yaani sheria zake ni nyepesi sana. Yesu hana Sheria kama Ibirisi alivyo na sharia Ngumu, sheria za ibirisi ukienda kwa mganga wa kienyeji atakwambia ili utajirike mtoe mkeo kafara au mwanao Yule unayempenda sana ndipo utajiri uupate. Lakini kwa yesu ni rahisi tu, Biblia inasema mkabidhi Bwana njia zako naye atakupa yale ambayo moyo wako unayatamani, kama unatamani fedha anakupa tu wala hakuna shida, Biblia inasema Fedha na Dhahabu ni mali yake kwa hiyo atakupa bila shida.
Haijalishi ndoa yako inayumba sana yeye ukimkabidhi hiyo ndoa yako atairekesha mapema mno, haitayumba tena maana yeye anaitwa mshauri wa ajabu mfalme wa amani. kama amani ilikuwa imeondoka atairejesha, kama mumeo/mkeo hakusikilizi yeye atamshauri maana yeye ni mshauri wa ajabu atakusikiliza tena vizuri kabisa. Acha kuteseka mwambie Yesu akutue mzigo wako leo.
Bwana akubariki.
Ev.Moses Mayila

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s