ACHA KUWA NA MAISHA YA WASIWASI

 

SOMO: WASIWASI

Maandiko:MATHAYO 6:25-33

Wazo kuu: Mkristo hapaswi kuishi maisha ya wasiwasi

UTANGULIZI:

1.     Utafiti kuhusu wasiwasi

o   Kwa makadirio 40%  ya wasiwasi ni kwa mambo ambayo  huwa kamwe hajatokei

o   Karibu 30% ya wasiwasi ni kwa mambo ambayo yameshatukia na hayawezwi kubadilishwa

o   12% ya wasiwasi ni kwa mambo yanayo tupa wasiwasi  ni kuhusu uzima naafya na zetu-nikiumwa je? kweli nitapona?n.k

o   10%  ya wasiwasi ni kwa mambo madogo madogo sana yasiyo na umuhimu wowote kama vile watu wanatusemaye?,watu wanatuonaje?

o   8% ya wasiwasi ni kwa mambo  Ambayo kweli ni halisi na halali.

o   Hivyo  tunawasiwasi kwa asilimia 92% kwa mambo yasiyo na sababu za msingi na hii inatu maliza wenyewe.elekeza asilimia 92% ya muda na nguvu zako juu ya 8% ya mambo yakupayo wasiwasi ambayo ni halisi na halali na  utaweza kuyatatua kirahisi hayo matatizoyanayokupa wasiwasi.na utafurahi maisha, na kuwa na afya  na ufanisi zaidi katika  maishayako

 

2.      Kielelezo/mfano:

m  mwanamke  mmoja ambaye alikuwa halali vizuri kwa wasiwasi wa kuvamiwa usiku na wezi ,takribani kwa miaka kumi,siku moja ikatokea na kutimia sawa na wasiwasi wake,mwizi akavamia nyumba yao  na mume akafanya mzaha kwa tukio hilo akamkaribisha yule mwizi na kumsihi asikimbie maana hata mdhuru au kuita polisi,akamwambia subiri nimwite mke wangu ni muhimu akuone,kisha akamwamsha mke wake na kumwambia Mwizi wako uliyekuwa una mngojea kwa muda mrefu huyu hapa njoo umwone!

 Sermonic Explanation

Yesu anatufundisha kwamba hatupaswi kuwa na wasiwasi bali tutafute kwanza ufalme wake na hayo mengine yanayotupa wasiwasi Mungu Atashughulikia

Prepostion:

Watu wa Mungu wana weza kuishi bila  wasiwasi pamoja na changamoto zote wanazokutana nazo katika maisha kwa Kutafuta ufalme wa Mungu Kwanza. katika somo hili tutajifunza mambo manne kuhusu wasiwasi kwa kujibu maswali haya manne: Je,Wasiwasi ninini?.Je, wasiwasi ni Dhambi? Je,Dalili za wasiwasi ni zipi? Je,kwasababu gani ni siwe na wasiwasi?.Je,ninawezaje kushinda wasiwasi?

  1. Je,Wasiwasi ninini?
  •    Kuna uhusiano wa karibu kati ya hofu na wasiwasi ,ingawa wasiwasi sio hofu,bali hofu huweza kuzaa wasiwasi.mara nyingi wasiwasi ni matokeo ya hofu,
  •  Hofu ni hisia tunazo zionyesha wakati wa hatari iliyo dhahiri,wasiwasi ni hisia tunazozionyesha juu ya nini kinaweza kutokea lakini si halisi bado, lakini hofu jambo ni halisi,wasiwasi jambo bado si halisi.Watu Wote tuna wasiwasi  na hofu katika viwango mbalimbali,na kwa mambo mbalimbali tofauti
  • Wasiwasi ni hali ya kujali kupita kiasi juu ya masuala ya maisha,wasiwasi hutokea pale unapojali sana kuhusu matatizo ya maisha kiasi kwamba huwezi fikiri juu ya jambo jingine lolote.ni hisia za nguvu za hofu na kutokuwa na uhakika.
  • wasiwasi kama kitendo ni  kujitesa mwenyewe  au kuteseka kutokana na mawazo yanayokusumbua.Wasiwasi ni kama hadithi ya kutunga ambayo inaisha vibaya kwa kusikitisha,ni ya kutunga kwasababu si kitu halisi kilichotokea(fiction).wasiwasi ni hali au (jambo )unayoitunga wewe si hali halisi bado kwa wakati huu,na mara nyingi haitimii kuwa halisi                          

Je ni kwasababu gani ni siwe na wasiwasi

  •  Wasiwasi hukamilishi jambo lolote

o   Wasiwasi na kufadhaika hakuondoi matatizo ya kesho,sana sana kuna kuna tumaliza nguvu zetu za kuyakabili matatizo yetu ya leo.utajikuta huna uwezo wa kubebe mzigo wa leo kwasababu tayari umelemewa na matatizo yakutarajiwa ya kesho.

Wasiwasi unavuta mawingu ya kesho juu ya mwangaza wa jua wa leo

o   Wasiwasi ni sawa na “Dense fog”- Ukungu mzito unaoweza kufunika eneo la block 7  la ,mitaa 7 kwa ft100  kama ukikusanywa wote haujai zaidi ya Glass moja ya maji!,lakini unagawanyika katika matone madogo madogo 60,000,000,na kufunika eneo kubwa,ndiyo ulivyo wasiwasi,tukikusanya wasiwasi wetu wote tutona  picha halisi ya kushangaza ni asilimia 8%

Wasiwasi  si mzuri kwa Afya yako

Wasiwasi ni Kinyume cha kumtegemea Mungu

Sababu moja wapo kwanini tuna wasiwasi sana ni kwasababu hatuna uwezo wa kutawala  mazingira ya maisha . Tabia moja wapo ya wasiwasi ni hii

Wasiwasi huvikuza na kufanya mambo yasiyo na umuhimu kuwa na kivuli kikubwa. Siku zote wasiwasi huvipa vitu vidogo kivuli kikubwa. kuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho bado hakijatokea na kinaweza kisitokee ni kuteseka kwa ziada kwa kitu ambacho kamwe kinaweza kisitokee

Wasiwasi unaelekeza mtazamo wako upande usio sahihi MATHAYO 6:25,30-33

 

    III.            Je wasiwasi ni Dhambi?

kwanini ninini wasiwasi ni dhambi?sababu  zifuatazo

A.    Wasiwasi unamwondoa Mungu katika nafasi yake katika maisha yako,ni kuishi kana kwamba Mungu hayupo na ni kuishi kana kwamba upo pekee yako na pekee yako utatatua haya matatizo.

B.     Wasiwasi ni kudhania unafanya majukumu ambayo Mungu ajakupa,ni kuchukua nafasi ya Mungu na kujifanya Mungu,ni kutaka kutawala yasiyotawalika.

C.     Wasiwasi ni matokeo ya kukosa Imani,ni kuwa na Imani haba  MATHAYO 6:30 Wasiwasi una kuvuta toka katika mambo ambayo ni ya muhimu katika maisha.kadiri unavyokuwa na wasiwasi,huwezi kufanya chochote,unakabwa na wasiwasi.

D.    Wasiwasi ni Imani kwa upande Hasi,ni kutegemea mabaya,ni kuwa na hakika juu ya maafa,na nikuwa na imani katika kushindwa.Mwanzo wa wasiwasi ni mwisho wa imani,mwanzo wa imani ya kweli ni mwisho wa wasiwasi

 IV.            Je,Dalili za wasiwasi ni Zipi?

Utajuaje kwamba hali ya kimsingi na ya kihalali ya kujali mambo Fulani ya maisha imevuka mpaka na kugeuka  kuwa dhambi ya wasiwasi?

A.    Ni pale jambo ambalo unalijali linakuwa ndilo la kwanza unalolifikiria asubuhi na la mwisho unaloliwaza usiku kabla ya kulala.

B.     Ni pale Unapojikuta mwenyewe unalifikiria kila wakati wa akiba unapopatikana

C.     Ni pale Unapojikuta  unalileta hilo jambo katika kila mazungumzo yako.

    V.            .Je,ninawezaje kushinda wasiwasi?

A.    BADALA YA KUWA NA WASIWASI  OMBEA  KILA JAMBO LINALOKUPA WASIWASI:  WAFILIPI 4:4-6 Hakuna ombi dogo,lolote linalokufanya uwe na wasiwasi ni kubwa tosha kuliombea.kama ni kubwa kukufanya uwe na wasiwasi basi ni kubwa kukufanya uliombee.Kuomba ni kukabidhi fadhaa zako mzigo yako kwa bwana 1Petro 5:7 hakuna tatizo ambalo ni kubwa sana kwa nguvu za Mungu au ni dogo sana Mungu kulijali.

B.     Kuna familia moja waliamua kushugulika na wasiwasi katika maisha yao,wakakubaliana  kuwa na mfano wa box la maombi jikoni na waka liweka mahali pa juu,kila ombi linaandikwa na kuwekwa humo.kila  kitu kinacho leta wasiwasi kinageuzwa ombi la kuombea;kanuni waliyoikweka na kukubaliana  ni ukianza tena kuwa na wasiwasi juu ya jambo uliliandika kama ombi basi utapanda juu na kulitoa karatasi la ombi hilo kwenye box.utaratibu huu uliwasaidia sana,pengine unahitaji kuuiga na familia yako!

C.     Shirika la Bima  moja nchini Marekani lilifanya utafiti,na kugundua kwamba wale wateja wao ambao walikuwa wana hudhuria kanisani angalau mara moja kwa wiki waliishi kwa wastani wa miaka 5.7 zaidi ukilinganisha na wale wengine wa kawaida.sababu  ni rahisi tu,wale wanaoenda kanisani wana uwezekano mkubwa wa kuombea matatizo yao badala ya kuwa na wasi wasi,kuliko wale ambao hawaendi kanisani.

D.    ISHI SIKU MOJA KWA WAKATI                                                                                    Usiwe na wasiwasi juu ya siku zijazo mbele MATHAYO 6:34 Kila siku ina matatizo ya kutosha yakufanya  uwe na shughuli nyingi,wewe shughulika na leo na Mungu ataishughulikia keshoSi masumbufu ya leo,bali  ni masumbu ya kesho ndiyo yana mkandamiza mtu na kumlemea.

E.     Inasemekani watu wa Alaska wanaoitwa waeskimo wana falsa hii juu ya maisha -Usimuulize Eskimo juu ya umri wake,atakuambia ni sijui na sitaki kujua,ukimbana sana atakuambia  umri wangu ni “kama siku moja hivi” siku ikiwa hijaisha. Wanamaanisha nini?wao wana imani  ya kwamba wanapoenda kulala usiku wamekufa,wakiamka asubuhi wamefufuka na siku mpya na maisha mapya,hivyo kwao hakuna aliye na zaidi ya mwaka mmoja.kutokana na mazingira magumu wanayoishi ya baridi kali na theluji wamejifunza kuishi siku moja kwa wakati.pamoja na mzingira magumu ya maisha yao ni nadra kumkuta mwenye wasiwasi na kufadhaaika.

F.     Dhamiria kuishii leo,kesho mwachie Mungu.ishi siku moja kwa wakati Tunaweza kumudu kwa urahasi kama tu tutachukua mzigo uliopangwa kwaajili ya siku hiyo,lakini mzigo utakuwa mzito zaidi kama tutabeba na mzigo wa jana juu ya mzigo wa leo na kisha kuongeza tena mzigo wa kesho ambao hatuja pangiwa kuubeba leo. Uamuzi ni wa kwetu,tunaweza amua kuazima matatizo ya kesho leo,na kuishi kama vile Mungu hayupo au tukamwamini na kumtafuta kwa mioyo yetu yote.

Hitimisho:

o   Kuwa na wasiwasi kuhusu siku za usoni ni kama kuaanza kulipia riba sasa kwa mkopo ambao utauchukua mwakani.malipo unayo yafanya hapa katikati yana pote bure!Na bado ukichukua mkopo itakulazimu kulipa kiasi kamili cha riba kwa mkopo uliochukua,maana yake malipo uliyolipa kabla yamepotea bure na wakati huu huna fedha ya kulipia malipo yanayokukabilisasa.

o   kimsingi tunachotupa wasiwasi ni kivuli kikubwa cha matatizo.tunaogopa kivuli na siyo tatizo halisi. Ukiyaangalia maisha kupitia mawani ya wasiwasi matatizo utayaona ni makubwa kuliko yalivyo. Hesabu 13:24-33-haya kuwa majitu kwa ukubwa ule waliousema,ila wasiwasi wao ulifanya majitu yaonekane ni makubwa kupita uhalisi wake.

o   kuwa na wasiwasi juu ya kile ambacho bado hakijatokea na kinaweza kisitokee ni kuteseka kwa ziada kwa kitu ambacho kamwe kinaweza kisitokee. Methali ya kiscotch-kile kinachoweza tokea,kina weza kisitokee-what may be-may not be

o    Mtu mkuu wa Mungu mmoja alisema hivi“Kuna siku mbili katika wiki ambazo katika hizo na juu ya hizo kamwe si sumbuki nazo ..jana na kesho”

o   Kuwa na wasiwasi hakuna faida yoyote,hakuwezi kubadilisha yaliyo pita wala kuyatawala mambo ya siku ziajazo, kwa nguvu zako,ni kupoteza ubunifu.tunapokuwa na wasiwasi juu ya jambo Fulani,wasiwasi hulifanya lionekane kubwa zaidi kulivyo uhalisi wake.

Mungu akubariki na wasiwasi usiwe na sehemu katika maisha yako,tendea kazi somo hili na

maisha yako hayatabaki vile yalivyo .

katika Kristo

Pastor/Teacher- Mtitu M.A. jr 

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to ACHA KUWA NA MAISHA YA WASIWASI

  1. Jeremy says:

    Thanks Pastor, Bwana akubariki sana kwa somo zuri.

    Like

  2. Meinrald says:

    Asante.

    Like

  3. joseph says:

    asante sana kwa neno zuri limenipa moyo kwan nipo katika kipindi kigumu sana wasiwasi mwingi juu ya maisha yangu………………………………..

    Like

  4. H. J. Brown says:

    Thanks , I’ve recently been looking for information about this topic for a long
    time and yours is the greatest I have found out till now.
    But, what about the bottom line? Are you positive in regards to the supply?

    Like

Leave a comment