ASANTENI SANA MLIOMBA KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI, MGOMO UMEKWISHA NA MADAKTRI WAMEREJEA KAZINI TENA

Shalom ndugu zetu!

Tunawashukuru sana nyote mliojitoa kuombea Tanzania, kwani mgomo wa madatkari umefikia mwisho hapo leo baada ya Rais Kikwete kuzunguma na madktari na kupata muafaka. hivyo madaktari watakuwa kazini kuanzia kesho. Bwana awabariki sana mlioomba kwajili ya hilo. Lakini pia tusinyamaze tuendelee kuombea Tanzania, maana iko migogoro mikubwa kuliko hii inaweza kutokea wakati wowote kama Mungu asipo simama, lakini wakati mwingine inakuwa vigumu kwa Mungu kusimimamia nchi yenye kuasi kama hii. Tanzania ni nchi isiyomjua Mungu, Serikali yake haitambui mambo ya Mungu, naweza kusema Serikali ya tanzania inakiburi juu ya Mungu,na kiburi hiki kinaweza kufananishwa na kiburi cha Moabu. Bwana Mungu anataka serikali zote zimuheshimu lakini Tanzania jambo hilo halipo. Katiba inasema Nchi haina Dini ila watu wake ndio wanadini, kwa maana nyingine ni kwamba nchi haina Mungu ila watu wake ndio wana Mungu. sasa jamani kwa sababu sisi watanzania tuna Mungu, basi na tusimame na hiyo nguvu ya Mungu wetu hata tulete mabadiliko katika nchi. mimi najua mambo haya yanatokea kwa sababu taifa halimwombi Mungu, hata viongozi wanapokuwa madarakani hawaongozi kwa mujibu wa sheria za Mungu, bali kwa mujibu wa akili zao na katiba ya nchi isiyo na Mungu.

Hivyo Mungu yuko mabali nasi wala hashughuliki sana nasi, ndio maana shetani anaikoroga nchi, anaipepeta kama mchele! kwa sababu taifa halimwombi Mungu hata wakati wa kuchagua kiongozi Bora, tunajikuta tunaongozwa na viongozi wezi, walafi na mafisadi. wizi wa mali za serikali unaongezeka kila leo, wala hapana haki mahakamani. lakini haya yote ni matunda ya kile alichofanya mwalimu nyerere pale Bagamoyo wakati wa kutwaa uhuru. Nyerere alifanya matambiko ya kishetani ili apate uhuru, kwa hiyo mwangalizi wa nchi hii siyo Mungu bali ni shetani aliyeipa nchi uhuru. Laiti kama watu hawa wangenisikia na kuacha nyendo zao mbaya, wakabadilisha mfumo wa katiba hii, wakakabidhi nchi mikononi mwa Mungu, nchi hii itaenda vizuri sana. Angalia mfano mzuri taifa la Marekani, taifa hilo lilianzshwa na watu wa Mungu, wakamwomba Mungu kisha wakamkabidhi mungu nchi yao, ndiyo maana hata fedha yao imeandikwa (In God we trust) yaani twamwamini Mungu.

Marekani ndiyo taifa lenye nguvu duniani kwa sasa, nguvu ya marekani haitokani na teknolojia zao, bali yatokana na Mungu kwa sababu Bwana amekabidhiwa taifa. Tanzania Amka sasa, mwambie Bwana afanye mapinduzi, serikali hii ibadilishe katiba yake, iwekwe katiba yenye kutambua uwepo wa Mungu. Lakini haya yote yanawezekana kama utamwomba Mungu sawa sawa, tafadhali inua macho yako sasa, sema na Bwana Mungu muumba wako, ili Bwana aiponye nchi, Biblia inasema watu wangu wakijinyeyekeza kwa jina langu, wakatubu nami nikasikia kutoka mbinguni, nitawasamehe dhambi zao. Ungana nasi, kuwaombea viongozi wetu na nchi yetu kwa ujumla. ili Mungu awawezeshe viongozi kumjua yeye na nchi ipate mwangaza.

Bwana Isaidie Tanzania, Mungu wasaidie viongozi wetu.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s