Na. Mch. Josephat Gwajima Mwachie Aliyetumwa..

19.feb 2011
Somo. Mwachie aliyetumwa.

Kutuma- ni hali ya kupewa ujumbe kwa ajili ya kupeleka palipo kusudiwa. Unaweza ukawa ujumbe wa familia au nchi. Mungu naye Ana kawaida ya kuwafumba watu duniani na Jumbe mbalimbali…

Maandiko yanayotaja uweza wa Mungu wa kutumia watu.
Kama hutaki matatizo mwachie aliyetumwa, kwa desturi Mungu huwa anatuma watu duniani na hii ni desturi ya Mungu. Yeremia 49:14 . Na hawa watu hutumwa kwa makusudi mbalimbali Kutoka 23:20 malaki 3: 1, mathayo 11:10 , watu wa dunia hii kwa kumuonea mtu anakupa pamoja nao, au anaishi katikati Yao huisikia kuwa hajatumwa, lakini hata kwenye biblia watu waliotumwa walikuwa wanaishi na kula kama watu wengine.

mifano ya watu waliotumwa kwenye biblia.
Marko 1:2 huyu ni Yohana mbatizaji, alitumwa kuandaa njia kwa ajili ya Yesu .
Hata Yesu mwenyewe alikuwa ametumwa Kutoka mbinguni lakini alitungwa mimba, akazaliwa, na Akaishi Kama watu wengine, Hesabu 20:16 Mungu anatabia ya kutumia. 2Samweli 12:1 zaburi 105:26. Mathayo 21:37 waamuzi 6:28 Mungu anatabia ya kutuma watu.

Mfano wa wanasayansi.
Wanasayansi wengi wa zamani amabao walikuwa wakristo na ni wavumbuzi wa zamani wa sayansi, mfano 1. isaack newton, 2. Boyle, na watu Kama wakina 3. kelvin waliogundua umeme hawa watu walikuwa wameokoka na hawa waligundua vitu mbalimbali. 4. Michael faraday Kama tulivyoona wagunduzi wa zamani wengi wanakubali kuwa Mungu yupo. 5. John Rey, 6. Creg Maxwell 7. Caros Linus, 8. Kepler. waliokuwa wameokoka.

Lakini ukiangalia maisha yao binafsi, utagundua maisha yao yakipita mambo magumu,
Mfano: isaack newton mama yake akiwa mjamzito, baba yake akafariki … Hivyo mama yake akaenda kuolewa na mume mwingine, Na hapo newto akaenda kuishi kwa mjomba yake na katika maisha magumu na kutokana na maisha magumu yale , yakamfanya newton akazane kusoma kumbe mtu aliyetumwa kuibadili dunia na hapa lazima dunia imshikilie na kumzuia, lakini mwisho wa siku alikwenda na kumaliza wito wake.
Mfano mwingine ni Robert Boyle naye alizaliwa kwenye shida pia, Faraday pia Alipitia wakati mgumu kwenye maisha yake.

Maisha halisi ya sasa.

Tunapozungumzia kutumwa ni neno pana sana na hapa inaweza ikawa mtu katumwa kubadili nchi, familia, nyumba na Hali ya jamii nzima. Lakini dunia hii tuliopo ina system mbalimbali mfano. Dini, serikari, jeshi ambavyo vinazuia ujumbe wa aliyetumwa. Marko 1:2 , “palitokea mtu ametumwa…..” unajikuta unakiu ya jambo fulani kufanikiwa, una kiu ya kufanikisha kitu fulani kinaweza kuwa cha familia au cha taifa na hapo hali ya maisha na umaskini ina kuzuia, na hii ni kawaida ya dunia kujaribu kuwashikilia watu waliotumwa..

Kumbe inawezekana kuwa Mungu amekutuma duniani, na hujijui na kwa vile dunia ilivyokushikilia inakufanya hata usahau kuwa umetumwa. Mfano: inawezekana umetumwa kuwa waziri wa mambo ya nje na hapo inakubidi upate elimu angalau, lakini dunia inakuzuia kwa kukuletea umaskini ili ukose elimu na mwisho wa siku ushindwe kufikia kwenye kule ulipotumwa.

Msaada kutoka kwa Mungu kwa Yule aliyemtuma.

Kama tulivyoona Mungu anadesturi ya kutuma malaika, binadamu ili kuitengeneza dunia kuishape dunia kuileta mahala pake… Na Mungu ili kuwasaidia aliowatuma huitikisa dunia kwa jambo fulani ili kufanya wale aliowatuma waingie kwenye system, na hapa ndio maana unaona hata nchi Kama Tanzania inapitia kwenye mtikisiko ikionyesha kuwa kuna watu waliotumwa na wanakusudiwa kuingia kwenye nafasi zao.

Mfano mwingine ni wa Ibrahim , ambaye ni baba wa Imani, na huyu aliahidiwa kuwa baba wa mataifa na ili kuwa baba wa mataifa lazima azae awe na watoto, lakini dunia( shetani) akaanza kupinga hiyo, kwa kumwekea utasa, na hapa tunajifunza kuwa kwa kila mtu aliyetumwa lazima atakutana na upinzani.

Mfano mwingine ni Musa , na Musa alipozaliwa tu , shetani akajua na alitumwa na Mungu kuunda taifa imara, la Israel na ndio maana alipozaliwa tu, Farao akaamuru watoto wote waangamizwe, na hapa tunajifunza kumbe ukiwa na kitu kikubwa cha Mungu , lazima utapingwa na kuzuiwa. Lakini Musa kimuujiza alienda kula mezani mwa Farao. Bila Farao kujua hadi wakati wake hutimie.
Kumbe aliyetumwa hawezi kuangamizwa hadi atimize hatma yake.
Kwahiyo Mungu anakwaida ya kuwasaidia wale aliowtuma, tunaona katika habari ya Musa alipokuwa mdogo, na hata yale mapigo aliowaandalia wamisri,

Mfano mwingine wa taifa la Israel, kipindi Sauli alipofanya machukizo… Mungu akamtuma nabii Samuel kwenda kumpaka Mafuta mfalme Daud . Mungu anakawaida ya kutuma watu. kwa hiyo samweli akamchagua na kumtia Mafuta daudi.
Vitu ambavyo vilimshikilia Daud Kama mpakwa mafuta.
1. Kudharuliwa na ndugu zake.
2. Yuko machungoni polini.
3. Alidharauliwa na watu wa taifa lake.
Lakini pamoja na yote daudi aliishia kuwa mfalme sawasawa na alivyoitwa.

Jambo la kufanya:
Ni muhimu kupambana vita vya kiroho ili kuondoa vizuizi vya dunia, ambavyo vinazuia watu waliotumwa… Kwa hiyo ni muhimu kusambaratisha nguvu ya shetani ili kutuachia watu tuliotumwa.
Writer: davidmgongolwa@ymail.com

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

5 Responses to Na. Mch. Josephat Gwajima Mwachie Aliyetumwa..

  1. Peter says:

    Ndugu wapendwa katika Bwana,
    Napenda kuwajurisha kuwa usiku wa juma mosi kaka yetu marehem GREGORY PROTACE alimtokea mdogo wake DEOGRATIAS PROTACE na Kumuuliza kwanini walimuua? Huyu DEOGRATIS ndiye mwenye mke anayesadikiwa kumuua kaka yetu GREGORY.Tafadhari sana ninawaomba mzidi kuomba ili kumkomboa kaka yetu mpendwa.Ahadi yangu baada ya kumkomboa kaka kutoka mikononi mwa shetani ni kuokoka mimi na familia yangu yote na familia ya kaka yetu. Ninawaomba mnisaidie.

    Ishengoma.

    —–Original Message—–
    From: Ishengoma, Peter [ICG-GTS NE]
    Sent: Friday, March 02, 2012 3:35 PM
    To: ‘prayer@ufufuonauzimaministries.org’
    Subject: THE DEATH OF MY ELDER BROTHER GREGORY PROTACE

    Dear Ufufuo na Uzima Ministries (GCTC) or (Majeshi ya Ufufuo)

    It is with much feeling that I received a bad news of my sad loss, My Elder brother GREGORY PROTACE NIWAGIRA he has passed away on Friday January 13,2011 at Rubya Hospital Muleba Kagera Region after short sickness .

    The burial of our beloved elder brother was taken place on Sunday January 15, 2012. at Buyera village.
    It is truly an irreparable loss. I feel the blank so much. I can yet hardly believe it is true. I have indeed been comforted by the knowledge that all was done for the best by the Divine wisdom . I know that God will relief my pain for is the Merciful One.
    Kindly assist to return him alive so that he may live a victorious life. Glory be to God. I desire to see the Holy Spirit’s miracle-working power.

    Thanks and Best Regards

    Ishengoma.

    Regards
    Peter Ishengoma.
    Cell. 0717 658610 / 0788 658610 / 0757 315899

    —–Original Message—–
    From: Ishengoma, Peter [ICG-GTS NE]
    Sent: Monday, February 27, 2012 3:04 PM
    To: ‘info@ufufuonauzimaministries.org’
    Subject: KIFO CHA KAKA YANGU GREGORY PROTACE

    Mchungaji Joseph Gwajima,

    Ninakuomba sana utumie uwezo na karama ulizopewa na mwenyezi Mungu umurudishe kaka yangu GREGORY PROTACE aliyefariki
    Tarehe 13/01/2012 katika Hospital ya Rubya Muleba Kagera na kuzikwa kataka kitongoji cha Buyera mnamo tarehe 15/01/2012.
    Kifo chake ni cha utata mtupu hadi kusababisha nyumba tatu za watu wanaosadikiwa kuwa wachawi kuchomwa moto na mmoja wapo
    Kufariki.

    Ninakuomba sana utusaidie.

    Peter.

    Like

  2. be blessed , first for making Jesus as the only pillar to depend on! According to the book of Isaiah 42:22 …. explain a lot about this and you have to know that God is God of restoration, he did for Lazarus he will do also to your beloved sister,! just put you are whole trust in him he can do exceedingly, abundantly above all you can think ..never give up! utampata ndugu yako….. welcome Ufufuo na Uzima ..worshiping at Tanganyika Packers, Kawe , Dar es salaam

    Like

  3. I think everything said made a lot of sense. But, think about this, what
    if you composed a catchier post title? I am not saying your information isn’t good., but suppose you added something that makes people want more? I mean Na. Mch. Josephat Gwajima Mwachie Aliyetumwa.. | NEW HOPE MINISTRY is a little plain. You should peek at Yahoo’s home page and watch how they
    create article titles to grab viewers interested.

    You might add a related video or a pic or two to grab people interested about everything’ve written. In my opinion, it could make your blog a little bit more interesting.

    Like

  4. buxtalk.com says:

    This website really has all of the information
    I needed about this subject and didn’t know who to ask.

    Like

  5. Lwadurha Esaie says:

    Jambo katika jina la Yesu . Ninge tamani nipate adress E- mail Yako binafsi ao ta huduma Yako Nina suali binafsi laku ongelea kwa ujasiri Tuna kufuata kupitia YouTube huku Marekani .Aksante

    Like

Leave a comment