Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima. Tarehe 17.6.2012

Ujumbe: VIUMBE NA MAUMBILE HEWA.

UTANGULIZI:-

Viumbe ni vilivyo umbwa , vyaweza kuwa wanadamu, vitu maji, anga na vitu vingine vyote, na Mumbile ni mtazamo wa viumbe hivyo. Ni Muhimu kujua viumbe vinapokuwa rohoni vinaweza kuvaa maumbile tofauti. Ndio maana kipindi Yesu amefufuka , Mariam mama yake alimuona na kuhisi ni mtunza bustani utajuuliza kwanini mama yake hakumtambua, hii ni kwasababu Yesu alijibadili na kuwa kama mtunza bustani, na mariam akahisi ni mtunza bustani.

ROHO ZINAWEZA KUVAA MAUMBE : Kibiblia:-

Unaposoma kitabu cha mwanzo ni muhimu kujua kina onyesha asili, mwanzo wa vitu vyote, sasa tuangalie kwa undani. MWANZO 3:1-24.. HII NI HABARI YA Adamu na Hawa walipokula tunda, katika mstari wa 13 “nyoka alinidanganya” na nyoka huyu ndo yuleyule shetani alibadili umbile lake,. kumbe biblia inasema toka asili (kitabu cha mwanzo) kinaeleza kuwa kuna uwezekano wa mtu wa rohoni kujibadilisha. Kumbe biblia inasema katika kitabu hiki kuwa toka mwanzo shetani wa rohoni aliwahi kujibalilisha na kuwa shetani.

Maandiko yanayoonyesha uwezekano huo:-
• ZABURI 91:13 utajiuliza kwanini biblia inasema utakanyaga nyoka, au samba .. ukichambua kwa akili ya rohoni jambo hili utagundua kumbe biblia inaonyesha uwezekano wa viumbe wa rohoni kuvaa miili.
• LUKA 10:19 Biblia inaonyesha maumbo, kumbe unaweza kuona mtu anasema.. tangu ameumwa na mdudu au alipokutana na mdudu, ndipo ugonjwa ulipoanzia” na Mungu kwa kujua uwezekano akatupa hili andiko kuwa tuna mamlaka ya kukanyaga nyoka na Ng’e. kwahiyo tunamamlaka juu yao.
• MARKO 16:18 kumbe hata kama ukinywa kitu ambacho kina sumu, au shetani kajibadili kuwa sumu basi hutakufa.
• ISAYA 27:1 Kumbe Biblia inaonyesha kuwa kunanyoka aliye baharini na ndio maana utaona kuna ajali zinatokea baharini, kumbe kuna shetani limejigeuza na kuwa joka baharini.

mara nyingi shetani hutenda kazi kwa kujibadilisha na kuwa kiumbe chochote ili kukuangusha, au kukufuatilia, kukutoa kwenye agano la Mungu. Ni muhimu kuwa makini kama mtu auliyeokoka na mambo haya kwa kuwa shetani aweza kujibadili maumbile mbalimbali.

SHETANI AWEZA KUJIBADILI MAUMBILE MBALIMBALI

Shetani anaweza kujibadili maumbile kwa ajili ya kutimiza azma yake aliyoikusudia, shetani akiamua kumteka mtu anaweza kutumia mtu, kitu, mti , gari au kitu chochote kutimiza azma yake. Na ndio maana Joshua alipokutana na mtu asiyemjua akamuuliza “je wewe ni wa upande wetu” Na mtu huyu alikuwa rohoni si mwilini tunaweza kuona katika kitabu cha JOSHUA 5:13-15 , Joshua alijua kuwa kuna uwezekano wa shetani kujibdili katika maumbile mbalimbali. Ndio maana kwa watu walioko mikoa ya shinyanga wanajua kunavijiji wanavyoita Gamboshi, ni miji yenye watu lakini ya kichawi, yaani mapepo na mashetani wamejibadili na kuwa mji. Kumbe shetani aweza kujibadili.

KUTOKA 8:6-7 tunaona hapa kuwa Haruni alinyoosha fimbo na kutokea vyura, juu ya nchi ya Misri, na waganga wa misri wakafanya vilevile kuleta vyura juu ya nchi, utajiuliza kwanini hawa waganga waliweza kuleta vyura.. ni kwasababu shetani anaweza kujibadili kwenda kwenye maumbo mbalimbali.

UFUNUO 13:10.. Yohana aliona katika ulimwengu wa roho, maumbo ya wanyama mbalimbali yote hii ni kudhihirisha kuwa shetani anaweza kujibadili, UFUNUO 13:6.. shetani hapa ameonekana kama mnyama aliyetoka baharini, kimsingi yeye shetani ni roho lakini anaweza kuvaa maumbo mbalimbali ili kutenda kazi katika kutimiza azma yake. Ni muhimu kukataa na kuangamiza maumbo yote ambayo shetani anatumia ili kukushambulia. “deactivate them in The Name Of Jesus”

Na ndio maana ni rahisi mtu kukwambia, ugonjwa ulimwanza baada ya kupaliwa.. kumbe shetani amegeuka na kuwa kitu cha kumpalia mtu ili kupitisha ugonjwa huo na kumfanya mtu ahisi kuwa kile kitu ndio kimesababisha. Hata kipindi cha Yesu walipokuwa wanavuka baharini na mashua ukaja upepo mkali na ukataka kuangusha kile chombo, lakini Yesu akaukemea na upepo ukatulia. Kimsingi Yule ni shetani alijibadili na kuwa upepo ili kuwazuia wasihubiri injili.

MIJI YA ROHONI.

UFUNUO 21:2 hapa tunaona kuwa Yohana aliona mji wa rohoni. Ufunuo 21:10 huu mji ambao Yohana aliona na haupo kwenye ulimwengu wa mwili na huwezi kuuona kimwili. Huu mji sio wa mwilini kwasababu Yohana akasema “ akanichukua katika roho” maana yake hakuwa katika ulimwengu wa mwili bali wa Rohoni. Na ndio maana hata shetani huiga “imitator” na kufanya miji duniani ili kuendesha shughuli zake. Ndio maana watu wengi wanaokufa katika mazingira ya kutatanisha “misukule” nao hupelekwa kwenye hiyo miji.

Hata kuzimu ni mji wa rohoni, ambao Yesu alipokufa alishuka kuzimu nakumlaani shetani, kuzimu ni mji wa rohoni. UFUNUO

USHINDI DHIDI YA VIUMBE HEWA.

1. Tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na nguvu zote za Yule muovu, wala hakuna kitu kitakacho kudhuru kwa namna yoyote ile.

2. Pia twaweza kuwashenda viumbe wa rohoni kwa kunena kwa lugha mara kwa mara, ambapo unamruhusu Roho mtakatifu akupiganie, hivyo viumbe vya ajabu vitajikuta vinajitenga na wewe.

3. Maombi pia ni silaha Kubwa dhidi ya viumbe vya hewa. Maombi yanalazimisha viumbe hivi kuondoka mahali ambapo walianza kujijenga kwa muda mrefu. Maombi yanauwezo wa kuangamiza ngome.

4. Sisi ni lungu la Bwana ambaolo kwa sisi, Mungu hufyeka farasi na mpanda farasi(viumbe hewa) kumbe hakuna wakufyeka ila sisi tuliookoka.

Somo hili linaendelea j3 hii kwa kuangalia kwa undani kuhusu miji hewa na vitu hewa. Isaya 19:18. Mji wa uhalibifu : – kumbe
kunauwezekano wa kuwepo mji kabisa katika ulimwengu war oho kwaajili ya uhalibifu. Kuleta uhalibifu.. katika ulimwengu waroho kuna miji lakini ya rohoni.

Mungu wetu ni Mungu Mtakatifu, wa upendo, hakuna kama yeye.. ni Mungu mkuu mno.. atufunuliaye mambo ya rohohoni maagumu tusiyo yajua.. na wala kuyawazia. MUNGU ANATUPENDA SANA.

Ufufuo na Uzima (The Glory Of Christ (T) Church)
Kawe, Dar es Salaam.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

8 Responses to Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima. Tarehe 17.6.2012

 1. Agnes says:

  asante baba , nimefuatilia tangu siku ya kwanza ya somo hili mpaka leo , nafurahi nazidi kubarikiwa katika jina la Yesu . Amen

  Like

 2. Asante Baba nimebarikiwa sana na somo hili.maoni yangu editing ziwe nzuri ilikuepuke kupoteza maana ya neno.

  Like

 3. Raphael says:

  Asante sana kwa somo zuri sana baba gwajima twasubilia mifuniko ya kichawi tupo pamoja katika kutenda kaziyake

  Like

 4. jane says:

  ubarikiwe sana

  Like

 5. jane says:

  mzidi kuongeza matawi mungu awabariki sana

  Like

 6. Elisha Cathbert says:

  AMEN nimejifunza mengi sana juu ya somo hili

  Like

 7. tunashukulu kwakutuweka sawa.

  Like

 8. Philemon Mc Duffy Phiri says:

  please could you give me your email address,there is something i wish to share with you very important

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s